25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Umeme wa ardhini kumaliza kero Temeke

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Tatizo la kukatika kwa umeme lililokuwa linaikabili Wilaya ya Temeke limepata ufumbuzi baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme chini ya ardhi.

Ujenzi wa huo wa msongo wa kilovoti 132 unagharimu Sh bilioni 16 na unatarajiwa kukamilika Machi 2024.

Akizungumza leo Februari 20,2024 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kukagua miradi ya maendeleo, Meneja wa Tanesco Temeke, Ezekiel Mashola, amesema njia hiyo yenye urefu wa kilomita 6.8 itazalisha megawati 100.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme chini ya ardhi katika Wilaya ya Temeke.

“Tunajenga njia hii ili kuhakikisha miundombinu ya umeme hailemewi kwa wingi wa umeme. Hadi Machi 30,2024 mgawo wa umeme Temeke utaisha,” amesema Mashola.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila, amesema ongezeko kubwa la uwekezaji hasa viwanda na makazi ya watu umesababisha njia za kusafirisha umeme kulemewa kwa kuwa miundombinu ya umeme ni ileile.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila, akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme chini ya ardhi katika Wilaya ya Temeke. Wanne kushoto ni Mbunge wa Temeke, Dorothy Kirave.

Amesema kupitia mradi huo wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme utamaliza mgawo wa umeme ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara katika wilaya hiyo hasa siku za Jumamosi na Jumapili.

“Umeme unapokatika kuna sababu zaidi ya moja na msichukulie jambo hili kisiasa, tusijadili mambo kwa mihemko. Kazi kubwa inafanyika na Rais Samia ametoa fedha ambazo zinatumika kujenga njia za kusafirisha umeme chini ya ardhi ikiwemo hii inayofanyika hapa…ujenzi utakapokamilika umeme hautasumbua tena,” amesema Chalamila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles