|Mwandishi Wetu, Mwanza
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali amesema serikali imeshaanza kutoa vibali vya kuagiza nyavu kwa utaratibu unaofaa.
Aidha, amewataka wavuvi kujiunga kwenye vikundi vya ushirika ili wapekelekewe mradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) wa Wavuvi Skimu.
Ulega amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara na wakazi wa Kisiwa cha Gana kilichopo wilayani Ukerewe alipofanya ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za wavuvi katika eneo hilo.
“Serikali inaratibu vyema upatikanaji vibali vya kuagiza nyavu bora kwa ajili ya shughuli za uvuvi, hivyo msiwe na wasiwasi, lakini pia jiungeni katika vikundi ili mradi huu wa NSSF utakaokopesha na uwasaidie kuimarisha shughuli zenu kupitia vikundi mtakavyoviunda,” amesema Ulega.
Hata hivyo, wakitoa maoni yao wavuvi hao walihoji kuhusu hatima ya samaki aina ya Furu, Gogogo, Nembe na Ningu ambao hawatajwi na sheria ya uvuvi.
Akijibu suala hilo Ulega amesema serikali inaanda muongozo utakaowasaidia kuvua samaki hao kwa uhuru.