LUGOLA AVITAKA VYOMBO VYA DOLA KUHAKIKI ARDHI INAYOMILIKI, KUILINDA ISIVAMIWE

0
971

|Bethsheba Wambura, Dar es SalaamWaziri wa Mambo wa Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amevitaka vyombo vya usalama na ulinzi nchini kuhakiki ardhi vinavyomiliki ili kujua ni ukubwa kiasi gani na viendelee kuwa imara katika kuilinda isivamiwe na watu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumanne Agosti 28, Lugola amesema uhakiki huo unafanyika baada ya kuwepo kwa uvamizi wa ardhi inayomilikiwa na vyombo hivyo kuvamiwa na wananchi na wawekezaji, kwa ajili ya matumizi yao binafsi.

“Navitaka vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuhakiki ardhi vinazoimiliki na kupima ili wapate haki miliki na viendelee kuwa imara na kulinda ardhi yao isimegwe na kuvamiwa na mtu yeyote.

“Ardhi inayomilikiwa na vyombo hivi imekuwa ikivamiwa na wananchi na wawekezaji, vyombo hivi ni muhimu na kadri siku zinavyoenda vinahitaji ardhi ya kutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali,” amesema.

Amesema ni marufuku kwa mwananchi yoyote kumega au kuvamia ardhi inayomilikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama na atakayeonekana atakuwa katika matatizo na misukosuko.

Amesema kuanzia sasa wananchi ambao wana mgogoro wa ardhi na vyombo hivyo ataanza ziara mikoani baada ya kipindi cha mkutano wa bunge na kufanya mikutano ya hadhara katika makao makuu ya mikoa ambapo amewataka wananchi kuwasilisha migogoro hiyo kwake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here