32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ukatili wa kijinsi; janga linalotesa Jeshi la Polisi

MWANDISHI WETU

TANZANIA bila ukatili dhidi ya wanawake na watoto, inawezeka.’ Hiyo ni kauli ya hamasa dhidi ya mapambano ya ukatili wa kijinsia ambao kwa nyakati tofauti hapa nchini umezidi kushika hatamu.

Licha ya kuwapo kwa jitihada mbalimbali kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na serikali kwa ujumla; hali ya ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto imeendelea kuharibu taswira ya nchi yetu kwa namna mbalimbali.

Ni jambo la kuhuzunisha kwamba sasa nyumbani ndiyo ma­hali penye hatari zaidi katika uhai wa wanawake kama ripoti ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu, (UNODC) iliyotolewa Novemba 25 mwaka jana ilivyobainisha.

Ripoti hiyo inasema ukatili na mauaji kwa wanawake wengi duniani wamekuwa wakipoteza maisha mikononi mwa wenzi wao au familia ambapo wanawake sita huuawa kila saa moja na watu wa­naowafahamu.

Hoja hiyo inaungwa mkono na ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) iliyotolewa Machi mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine ilibainisha kuwa zaidi ya visa 6,000 vya ukatili au unyanyasaji dhidi ya watoto iki­wamo ukatili kingono viliripotiwa mwaka 2018.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliopewa jina “Ukatili wa Kingono: Tishio kwa Haki na Ustawi wa Mtoto Tanzania” ilibainisha kuwa mambo yaliyoathiri haki za bin­adamu kwa mwaka 2018 ni pamoja na Sheria kandamizi, Ukatili dhidi ya watoto, hasa matukio ya mauaji na ulawiti wa watoto.

Hata hivyo, ili kuzuia muende­lezo wa matukio hayo ya kikatili, Jeshi la Polisi linatajwa kuwa kiungo muhimu katika kudhibiti na kuzuia kwa kushirikiana na wadau mbal­imbali.

Hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba polisi ndio wamepewa jukumu la kulinda raia na mali zao, lakini ili kudhibiti tabia na mienen­do isiyofaa ndani jamii, makundi mbalimbali kama vile viongozi wa dini, asasi za kiraia na wazazi wa­napaswa kushirikiana na jeshi hilo katika kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Kutokana na hali hiyo, Jukwa la Utu wa Mtoto (CDF) kila mwaka hukutana na Makamanda wa Polisi wa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la kuandaa mi­kakati, kutafakari na kupata mreje­sho kuhusu hali ya ukatili wa dhidi ya watoto na wanawake nchini. Pia kupeana uzoefu wa namna mbalim­bali wa kutatua kesi zinazoripotiwa katika vituo vyao vya polisi vya madawati ya jinsia na watoto kwe­nye mikoa yao.

Katika mkutano wa siku mbili uliondaliwa na CDF kwa kushiriki­ana Shirika la Idadi ya watu duniani (UNFPA), Ubalozi wa Sweden na Jeshi la Polisi umeibua mambo nyeti ambayo sasa yanapaswa kupigiwa chapuo ili yatekelezwe na kusaidia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Kuongezeka kwa matukio maana yake hujatimiza wajibu

Akizungumza na makamanda 38 walioshiriki mkutano huo hivi karibu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro anasema muendelezo wa matukio ya ukatili una maana kuwa kuna mahali kuna tatizo.

“RPC umepewa mkoa maana yake ni kuwalinda watoto, wa­nawake na watanzania wengine. Matukio haya yanaongezeka lazima kuna jambo maana yake hujatimiza wajibu wako,” anasema.

Anasema tathmini hiyo in­awaamsha wakuu hao wa polisi kuwa kuna mambo hawajatimiza.

“Hii ni changamoto ukikuta mtoto amebakwa au mwanamke amekufa ni changamoto kwetu kuwa kuna jambo halijakwenda vizuri.

“Juzi ni mashahidi mmepigiwa kelele sana, Njombe ilikuwa changamoto vilevile na Misungwi mtu mmoja wa hovyohovyo mjinga anataka kuwa tajiri anakwena kwa mganga mjinga anamuagiza ili uwe tajiri lazima auwe wanawake 59, na ameua hadi kufikia 29 ndipo na sisi tukamshughulikia.

“Ni lazima uache alama un­apokuwa kwenye mkoa kwa kuhakikisha uhalifu unapungua kwa kiasi kikubwa. Uhalifu ukiwepo na sisi tupo lazima kufikiri kwa kina,” anasema.

Aidha, anawaagiza makamanda hao kuhakikisha madawati ya polisi yanayoshughulikia matukio ya uka­tili wa kijinsia yanatumika ipasavyo ili kupunguza kadhia hiyo.

“Mtu akisema uhalifu umezidi lazima ujitathmini kwanini umezidi wakati mimi nipo, hivyo mkirudi badilisheni ufikiri wenu. Hizi changamoto zinarudisha nyuma utendaji wa makamanda. Nimeona leo niwapashe maana hamna namna,” anasema IGP Sirro.

Hoja hiyo inaungwa mkono pia na Mkuu wa kitengo cha Polisi Ushirikishwaji Jamii (CP) Mussa A. Mussa ambaye anasema changamo­to kubwa ni muda mwingi wame­kuwa wakisisitiza watu wafike kutoa taarifa kwenye vituo na kuacha umuhimu wa kuwaelimisha.

“Kwa muda huu tunataka tuwafikie wananchi sio kwa vipepe­rushi…tukae nao tuwafunze. Kuna changamoto za kiutendaji kama usafiri kulingana na jiografia ya nchi yetu lakini haya ni mambo ambayo tutayafanyia kazi,” anasema.

Anawaagiza makamanda wa polisi nchini kuenenda na mazin­gira ya mikoa wanayoiongoza kwa kuwa wasipojipanga vizuri makosa ya ukatili wa kijinsia yataonekana yanawashinda.

Anasema wasimamizi wa polisi jamii wawezeshwe ili waweze kufika kwa wananchi na kusikiliza matatizo yao.

“Madawati bado hayafanyi kazi vizuri, kuna changamoto ambazo sisi makamanda inabidi kuzitatua ili yafanye kazi vizuri. CDF mlifanya utafiti kidogo pia sisi tulifanya utafi­ti wa utendaji wa madawati haya, mliyosema na sisi tunayachukua na makamanda wataenda kuyatatua. Tunahitaji usimamizi madhubuti wa madawati.

“Kuna baadhi ya maeneo vifaa havitumiki ndani ya dawati, vinabadilishwa matumizi yake na matokeo yake madawati yanaachwa matupu. Au askari wa dawati ana­pangwa kazi nyingine.

“Madawati mengi askari wake ni wa kike, lakini wanatakiwa kuwa na mjumuiko wa wanaume.Tureke­bishe haya kwani dawati si kazi ya wanawake, kwa sababu wapo wanaume wanaopigwa na kudhalil­ishwa pia,” anasema.

Aidha, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa dawati la jinsia (SACP), Renata Mzinga anakiri kuwa mpaka sasa bado jamii inakumbwa na changamoto ya makosa ya ubakaji, ulawiti na kutelelekeza familia.

Anasema Serikali inafanya juhudi kuhakikisha jamii inakuwa sehemu salama kwa watu wa rika zote kwa kupitia madawati hayo ikiwamo kuchukua hatua kali kwa wale wanaoshiriki vitendo vya ukatili.

“Hili suala ni tatizo la kijamii hivyo jeshi linaendelee kutoa elimu kwa jamii. Jeshi hufanya kila jitihada kusambaza elimu kwa viongozi wa dini, mabaraza ya wazee na wa­nafunzi mashuleni ili kila mmoja

 Makamanda wazungumza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, (ACP) Hamduni Salum anasema asilimia kubwa ya matukio ya ubakaji, ulawiti na mauaji ya watoto yanatokana na imani za kishirikina.

“Matukio ambayo yame­pokelewa kuanzia Januari hadi Mei mwaka 2018 ni matukio hayo 423 wakati kipindi kama hicho kwa mwaka huu 2019 ni matukio 429,” anasema.

Anasema kuongezeka kwa namba ya makosa hayo kuna­tokana na uelewa wa wananchi hasa makosa ya ubakaji yaliyoku­wa hayaripotiwi.

Kaskazini Unguja

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja (SACP), Haji Abdalah Haji anasema mkoa huo ndio sehemu ambayo makosa mengi ya udhalilishaji kwa wa­toto ndipo yanapotokea.

“Usimamizi na ufuatil­iaji ndilo jambo la msingi kwa askari wetu kwa sababu jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu matukio haya. Tumewaita viongozi wa dini na wengine kuwaelimisha kwa sababu kesi za udhalilishaji haziwezi kuzuia na doria ya kipolisi lazima kuwe na doria ya kiroho,” anasema.

Katavi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi (ACP), Benjamin Kuzaga, anasema mkoa huo unakumbana na changamoto ya wahamiaji hususani jamii ya wafugaji kama vile wasukuma ambao hufuata malisho.

“Muingiliano huu umesaba­bisha mimba za utotoni lakini tunatekeleza azimio namba tatu la kuwashirikisha viongozi wa ngazi zote kutokomeza vitendo hivi,” anasema.

“Januari hadi Juni mwaka 2018 kulikuwa na makosa349 wakati mwaka 2019 kuanzia Januari hadi June yameripotiwa makosa 269,” anasema,

Kigoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma (ACP) Martine Otieno anasema mkoa huo unakabiliwa na tatizo la wakimbizi kutoka nchi za Burundi na Kongo am­bao hutekelezi vitendo vya ukati­li kwa kuwa tayari wameathiriwa kisaikolojia.

Pamoja na mambo mengine anasema hakuna ubakaji unao­fanywa na vijana wanaodaiwa kuitwa ‘teleza’ kama ilivyori­potiwa na baadhi ya vyombo vya

habari na mashirika binafsi.

Kilimanjaro

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (SACP) Hamisi Se­lemani anasema ipo haja sasa ya Bunge kubadilisha sheria inayor­uhusu watuhumiwa wa makosa ya kubaka kupewa dhamana ili kuondoa malalamiko dhidi ya Jeshi hilo kwa jamii.

“Lakini pia ni muhimu paanzishwe mahakama maalumu itakayoshughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kama zilivyo mahakama za mafisadi na ardhi,” anasema.

Iringa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (ACP) Juma Bwire anasema changamoto zinazok­wamisha vita dhidi ya ukatili wa kijinsia ni madaktari kukwepa kujaza fomu za PF3.

“Lakini pia waathirika wa­nakaa muda mrefu bila kuripoti polisi na pindi wanaposhindwa kukubaliana malipo labda ya ng’ombe ndipo wanakuja kuri­poti,” anasema.

CDF

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Koshuma Mtengeti anasema shirika hilo limetoa mafunzo kwa askari 270, kati yao wakiume 152 kutoka katika mikoa ya Mara, Dar es Salaam, Dodo­ma, Manyara na Kigoma.

“Kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA tumejenga madawati ya jinsi na watoto ikiwamo 22 yaliyopewa vitendea kazi. Lakini bado tunaomba Jeshi la Polisi linapowahamisha askari we­nye uweledi wa kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsi, pia lihakikishe linateua wale wenye utayari wa kushughulikia matukio hayo.

“Hali ya ukatili si nzuri kuna matukio mengi ya ulawiti, ubaka­ji, kumekuwa na kesi nyingi zinaripotiwa tunataka kujua ni hatua gani zinachukuliwa, lakini zaidi tunataka kujua ni jinsi gani wanachukua hatua za kuzuia matukio hayo na si kuripoti pekee,” anasema.

Hata hivyo, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Christine Kwayu anasema ili kuhakikisha ukatili wa kijinsi unatokomezwa, shirika hilo linaendelea kufanya tath­mini ya vituo 11 ili kuhakikisha kila kituo cha polisi kinakuwa na dawati la jinsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles