32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza kupata Waziri Mkuu mwanamke leo

Theresa May
Theresa May

LONDON, UINGEREZA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Theresa May, anatarajia kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza leo, akiwa na jukumu la kuongoza mchakato wa nchi hiyo kujitoa rasmi katika Umoja wa Ulaya (EU).

Hii ni baada ya mpinzani wake, Andrea Leadson kusitisha ghafla kampeni yake ya kuwania wadhifa huo.

May mwenye umri wa miaka 59, atamrithi David Cameron, aliyetangaza kujiuzulu baada ya Waingereza kupiga kura isiyotarajiwa, ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

May na Leadsom ilikuwa wachuane katika uchaguzi wa mashina wa Chama cha Conservative na matokeo kutangazwa Septemba 9.

Lakini Leadsom alijiondoa ghafla juzi baada ya kampeni yake kugubikwa na matamshi yaliyozusha utata kuhusu mpinzani wake kutokuwa na watoto na maswali iwapo alidanganya katika wasifu wake.

Akizungumza baada ya kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu mtarajiwa, May alisema: “Tunahitaji kuiunganisha nchi yetu na tunahitaji maono mapya yaliyo bora na imara kwa mustakabali wa nchi yetu.

“Maono ya nchi yetu yanayofanya kazi si tu kwa wachache wanaojiweza, lakini pia kwa kila mmoja wetu, kwa sababu tutawapa watu udhibiti zaidi wa maisha yao, na kuijenga Uingereza bora.”

Cameron aliongoza kikao chake cha mwisho cha Baraza la Mawaziri jana, na leo anatarajia kujibu maswali bungeni kabla ya kuikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Malkia Elizabeth.

May atakuwa Waziri Mkuu wa pili mwanamke nchini Uingereza baada ya Margaret Thatcher.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles