28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU: WAPINZANI WASUBIRI 2022 WAONGEE NA RUTO

NAIROBI, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta amepuuza wito wa kufanya majadiliano yoyote na kinara wa upinzani Raila Odinga kuhusu mageuzi ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, akisisitiza msimu wa chaguzi umekwisha.

Hilo limekuja huku shinikizo likizidi kumwandama Odinga asitishe mpango wake wa kesho kuapishwa kama ‘Rais wa Wananchi.’

Rais Kenyatta aliutaka muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) kusubiri hadi mwaka 2022 kufanya majadiliano ya kisiasa baada ya kumaliza hatamu yake ya uongozi.

“Siasa zimeisha, sasa ni wakati wa kuungana na kufanya kazi. Wale ambao wanataka mazungumzo wasubiri 2022 waongee na William (Ruto). Nitakuwa nimemaliza kazi yangu,” alisema Rais Kenyatta.

Akituhutubia waombolezaji wakati wa mazishi ya mama wa Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Murang’a Sabina Chege, Mama Susan Wairimu, Rais Kenyatta alibainisha kuwa atashiriki mazungumzo kuhusu mipango ya kuanzisha miradi ya maendeleo tu si mageuzi ya mfumo wa uchaguzi au siasa.

 

Mazishi hayo yalifanyika katika kijiji cha Kinyona eneo la kibunge la Kigumo kaunti ya Murang’a.

“Sasa yale mazungumzo ambayo tutashiriki ni ya maendeleo na uzalishaji nafasi za ajira kwa vijana. Tumemaliza siasa isipokuwa wale wachache ambao bado hawafahamu kuwa msimu wa siasa umeisha,” alisema Rais Kenyatta ambaye alikuwa ameandamana na Naibu wake, William Ruto pamoja na viongozi wengine wa eneo hilo.

Rais alikuwa akijibu wa wito wa viongozi wa NASA wa kutaka kuandaliwe mazungumzo kati yao na serikali kuhusu mageuzi wa mfumo wa uchaguzi huku wakijiandaa kumwapisha kinara wao, Raila Odinga kama ‘Rais wa Wananchi’ kesho wakati wa Sikukuu ya Jamhuri.

Wakati Kenyatta akisema hayo, Serikali ya Jubilee, wanadiplomasia, viongozi wa kidini na baadhi ya washirika wa NASA wamezidisha juhudi za kuhakikisha tukio la kesho la kuzindua Bunge la Watu halihusishi uchukuaji wa kiapo.

Hilo limekuja huku vyombo vya usalama vikifanya vikao namna ya kushughulikia tukio hilo baada ya hivi karibuni kushutumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi.

Wanadiplomasia wa Magharibui na Kanisa wanapendekeza uwapo wa mazungumzo baina ya Kenyatta na Odinga kutokana na uwezekano wa kutokea machafuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles