32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU AMLIZA RAILA KILA KONA

NAIROBI, KENYA

UHURU Kenyatta si kwamba amemshinda Raila Odinga katika nafasi ya urais pekee, bali hata kwenye kinyang’anyiro cha ugavana na useneta.

Baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuhitimisha matokeo yote, Muungano wa upinzani wa NASA ambao unajumuisha vyama vya Wiper, ODM, Ford Kenya, ANC, na PPK ulishindwa kufua dafu mbele ya chama cha Jubilee ambacho kimejizolea viti vingi katika nafasi ya ugavana na useneta.

Kaunti ya Nairobi, NASA ilipata viti vinane na Jubilee kimepata viti tisa.

Katika nafasi ya seneta, Jubilee kinaongoza kwa kupata viti 25.

Walioshinda viti hivyo na kaunti zao katika mabano ni Anuari Loitiptip (Lamu), Yusuf Haji (Garissa), Golich Juma (Tana River), Abdullah Ibrahim Ali (Wajir), Mohammed Maalim Mohammad (Mandera), Philip Salau (Kajiado), Susan Wakarura (Nakuru) na Onesmus Mukomen (Elgeyo).

Wengine ni Peter Njeru (Embu), Aaron Cheruiyot (Kericho), Wamatangi Kimani (Kiambu), Daniel Karaba Dickson (Kiriyaga), John Nderitu (Laikipia), Godana Hargura (Marsabit) na Irungu Kang’ata (Murang’a),

Katika orodha hiyo wamo pia Franklin Linturi (Meru), Johnson Sakala (Nairobi City), Cherarkey Samson (Nandi), Paul Mwangi (Nyandarua), Ephraim Mwangi (Nyeri), Steve Lelegwe (Samburu), Kithure Kindike (Tharaka), Michael Mbito (Trans Nzoia) na Margaret Kamar (Uasin Gishu).

Muungano wa upinzani NASA umepata viti 18 ambavyo vimekwenda kwa  Issa Juma (Kwale), Stewart Mwachiru (Kilifi), Enoch Kiio Wambua (Kitui), Mutula Kilonzo (Makueni) na Ladema Ole Kina (Narok).

Wengine ni Moses Masika Wetangula (Bungoma), Sitswila Amos Wako (Busia), Moses Otieno (Homa Bay), Cleophas Mallach (Kamamega), Samosn Ongeri (Kisii), Frederick Otieno Outa (Kisumu), Ben Enouch Okello(Migori), Mohammed Faki Mwinyihaji (Mombasa), Erick Mogeni (Nyamira),James Orengo (Siaya), Johnes Mwaruma (Taifa Taveta), Malachy Imana (Turkana) na Khaniri George (Vihiga).

 

NAFASI YA UGAVANA NASA vs JUBILEE

Katika nafasi ya ugavana vyama vyote vimegawana maeneo huku Jubilee kikiongoza dhidi ya NASA.

Jubilee kimepata magavana 25 ambao ni Stanley Kiplis (Baringo), Joyce Laboso (Bomet), Alex Tanui (Elegeyo), Martin Wambora (Embu), Ali Korane (Garissa), Joseph Lenku (Kajiado).

Wengine ni Paul Kipromo (Kericho), Ferdinand Babayao (Kiambu), Anne Waigumu (Kirinyaga), Salim Mgala (Kwale), Fahim Twaha(Lamu), Ali Ibrahim Roba (Mandera), Mohammed Mahmud Ali (Marsabit) na Kiratu Murungi (Meru).

Wapo pia Wa-Iria Mwangi (Maurang’a), Mike Sonko (Nairobi City), Lee Kinyajui (Nakuru), Stephen Kipyengsang (Nandi), Samuel Tunai (Narok), Francis Kimemia (Nyandarua), Patrick Gakuru (Nyeri), Moses Lenolkalal (Samburu), Onesmus Nyuki (Tharaka), Jackson Mandago (Uasin Gishu) na Mohammed Abdi Mahamud (Wajir)

NASA imepata magavana 18 ambao ni Wycliffe Wangamati (Bungoma), Sospeter Ojaamong (Busia), Cyprian Awiti (Homa Bay), Wycliffe Oparangah (Kakamega), Amason Kingi (Kilifi), James Ongwae (Kisii), Peter Nyong’o (Kisumu), Charity Ngilu (Kitui), Kivutha Kibwana (Makueni) na Zakaria Obado (Migori).

Miongoni mwa orodha hiyo pia wamo Hassan Joho (Mombasa), John Nyagarama (Nyamira), Cornel Amoth (Siaya), Graton Samboja (Taifa Taveta), Dhadho Godhana (Tana River), Patrick Khaemba (Trans Nzoia), Josephat Nanok (Turkana) na Wilber Ottichilo (Vihiga).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles