29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

UHAMIAJI KUTOA ‘PASSPORT’ ZA KIELEKTRONIKI

IDARA ya Uhamiaji inatarajia kutoa hati mpya za kusafiria (passport) za kielektroniki ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Septemba 13, katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala amesema uamuzi wa utoaji wa hati hizo za kielektroniki umetokana na makubaliano yaliyopitishwa na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutekeleza vigezo vya usalama kimataifa.

“Passport hizo zinatarajiwa kutolewa kuanzia miaka miwili ijayo,  na matumizi yake yataenda sambamba na passport za sasa hadi hapo hizi za zamani zitakapomalizika,” amesema.

Hata hivyo, Dk. Makakala amesema passport hizo za kielektroniki ni salama zaidi kwa kuwa zitakuwa na taarifa zote za mhusik na kwamba hayo ni baadhi ya maboresho yanayoendelea kufanywa na idara hiyo ili kuondokana na mfumo wa kianalojia na kuekelea kwenye mfumo wa kidigitali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles