Pyongyang, Korea kaskazini
Nchi ya korea kaskazini imetoa ripoti ya kuwa na uhaba wa chakula nchini humo.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wakati akihutubia maafisa wa ngazi za juu nchini humo.
Rais Kim alisema sekta ya kilimo imeshindwa kufikia malengo yake kutokana na tufani ya mwaka jana iliyosababisha mafuriko.
Pia kuna ripoti kwamba bei ya chakula imepanda, huku shirika la habari la Korea Kaskazini likiripoti kilo moja ya ndizi inagharimu dola 45 za Kimarekani.
Korea Kaskazini imefunga mipaka yake ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa vya Covid-19.
Biashara kati yake na nchi ya China imeporomoka sana kutokana na hatua hiyo Korea Kaskazini inategemea China kwa chakula, mbolea na mafuta.
Korea Kaskazini pia inajitahidi chini ya vikwazo vya kimataifa, vilivyowekwa kwa sababu ya mipango yake ya nyuklia.