22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuridhia mkataba wa kimataifa wa wafanyakazi wa ndani

Na Sheila Katikula,Mwanza

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani na kupinga usafirishaji haramu  wa binadamu ‘WOTESAWA’ lenye makao makuu yake jijini Mwanza limeiomba serikali kuridhia mkataba wa kimataifa wa haki za wafanya kazi wa ndani.

Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika Mkoani Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa WOTESAWA, Angela Benedicto alisema tangu mwaka 2011 serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania bado haijaridhia mkataba huo jambo ambalo huenda linachangia kuathiri haki za wafanyakazi wa majumbani.

Angela alisema ni miaka kumi sasa imetimia mkataba huo haujaridhiwa hivyo ni vyema uridhiwe kwa sababu ni daraja kubwa kwa wafanyakazi wa nyumbani kuweza kupata stahiki zao na haki za msingi kwa uhakika, kwa wakati na kwa kiwango sahihi ili kuwaongezea staha kwenye kazi zao.

Aliongeza kuwa, shirika hilo tangu mwaka  2012, limefanikiwa kuokoa takribani watoto 600 waliofanyiwa  vitendo vya ukatili na kuwarudisha  kwao  kwani pamoja na jitihada nyingi za serika kuhusu kulinda haki za watoto lakini bado kuna changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa zitatuliwe kisheria.

Aidha aliwaomba wadau kuendelea kutekeleza na kusimamia sheria na miongozo iliyopo nchini ili waweze kumlinda mtoto wa kike na kutoa wito kwa watanzania wanapoadhimisha siku hii kila mmoja kwa nafasi yake kukumbuka kusimamia mikataba na makubaliano ya kimataifa iliyowekwa juu ya ulinzi wa mtoto.

Alisema jamii kwa ujumla inapaswa kuguswa na aina yeyote ya ukatili dhidi ya mtoto na kuhakikisha inamlinda mtoto kwa kupaza sauti na pindi mtu anapoona mtoto anafanyiwa vitendo vya ukatili hatua kali zichukuliwe ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hizo za kunyanyasa watoto.

“Masuala haya yanapofika  katika ngazi ya mahakama waweze kutoa hukumu kwa wakati, kwa sababu tumeona Watoto wengi wanafanyiwa  vitendo hivi lakini mashitaka yanaenda taratibu na kupelekea watu kukata tamaa.

“Haki ya elimu iendelee kuzingatiwa kwa sababu ni bure kwani kuna baadhi ya  wazazi na walezi wamekuwa chanzo cha kutowapeleka watoto wao shule hawa nao waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ili watoto wapate  haki yao ya msingi kwa maana ya elimu.

“Leo hii tunaadhimisha siku ya mtoto wa afrika lakini pia ni Siku ambayo tunakumbukia shirika la kazi duniani  pamoja na wanachama wake chini Geniva lilisaini mkataba wa wafanyakazi kazi za staha kwa wafanyakazi wa nyambani,” alisema Angela.

Nae Meneja wa Shirika la Sos children Village Mwanza Dorothy Ndege alisema wameendelea kufanya kazi Kwa ukaribu na serikali na kwa nusu mwaka  wametumia zaidi ya shilingi million 100 kwa ajili ya miradi ya elimu na afya  ili kupunguza changamoto zinazowakabili watoto.

Alisema juhudi hizo zimesaidia  kupunguza changamoto si kwa watoto na kuweza kuhakikisha wanapewa hak zao na kulindwa kwani pamoja na juhudi zinazofanywa na asasi mbalimbali  watoto  hao wanatakiwa kujengewa mazingira ya kupaza sauti zao  waweze kujilinda wenyewe na kutosubiri kulindwa  ili kuhakikisha wanafikia ndoto zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya  Ilemela Dk Severini Larika  akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabliel ameitaka jamii kufichua  wazazi na walezi wanaotenda vitendo vya ukatili  kwa watoto wao Sanjari na kuacha usafirishaji haramu wa watoto kwani kufanya hivyo ni kosa.

Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika yanaadhimishwa huku yakiambatana  na kauli mbiu isemayo tutekeleze agenda 2040 kwa Afrika inayolinda haki za watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles