27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ugonjwa wa Zika janga la kimataifa

Ugonjwa wa ZikaJonas Mushi na Mashirika

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limetangaza hali ya dharura katika afya ya umma duniani na kuutangaza ugonjwa wa Zika kama janga la kimataifa kutokana kuenea na kusababisha  maelfu ya watoto   Brazil kuzaliwa wakiwa na ulemavu.

Pia shirika hilo limetahadharisha kuhusu ugonjwa huo kuenea katika mabara ya Asia na Afrika ambayo yana kiasi kikubwa cha watoto wanaozaliwa huku likiunda kikosi maalumu cha kimataifa cha kukabiliana na maambukizi mapya.

Ugonjwa huo umehusishwa na tatizo la kichwa kidogo (microcephaly) linalosababishwa na kutokamilika kwa ukuaji wa ubongo wa mtoto, tatizo ambalo limeenea  Amerika  Kusini  ingawa WHO imesema bado haijathibitishwa.

Jana Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Watoto wa WHO, Anthony Costello, alizungumza na vyombo vya habari huko Geneva Uswisi na kusema kimeundwa kikosi hicho ili kuwaleta pamoja watu wote mahali ambako shirika hilo lipo, makao makuu na kanda zote ili kuikabili Zika rasmi kwa kuzingatia fundisho walilopata wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

“Sababu ya kulifanya janga la kimataifa ni kutokana na hofu kwamba unaweza kuenea maeneo mengine duniani ambako watu hawajaanza kuchukua tahadhari,” alisema Costello na kuongeza:

“Tunajua mbu anayebeba virusi vya Zika wanapatikana  pia Afrika, Kusini mwa Ulaya na Asia hususan Asia Kusini.”

Costello alisema WHO inatayarisha  maelekezo mazuri kwa wajawazito na wakunga kutoa vipimo vilivyokubalika vya ukubwa wa kichwa cha mtoto ili kuwawezesha kubaini mtoto mwenye tatizo hilo.

“Kutoa elimu kwa watu wanaoishi maeneo yenye mbu na maeneo wanayofanyia kazi pamoja na uzalishaji mkubwa wa vifaa vya kufanyia vipimo ndio njia ya kukabili ugonjwa huu kwa vile chanjo inaweza kutuchukua miaka kadhaa,” alisema Costello.

Sanofi ambao ni watengenezaji wakubwa wa chanjo wamezindua mradi wa kutengeneza chanjo ya Zika hatua ambayo inaonekana ni uwajibikaji mkubwa katika kupambana na ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles