30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

UGONJWA WA MACHO WATESA WANANCHI MUHEZA

NA OSCAR ASSENGA- MUHEZA


ASIMILIA 90 ya wananchi Wilaya ya Muheza mkoani Tanga  wamekuwa wakikabiliwa na ugonjwa wa macho hasa kwa wazee kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Inaelezwa kuwa hali hiyo inachangiwa na hali ngumu ya maisha na hata kukosa fedha kwa ajili ya kumudu gharama za matibabu hospitali.

Kati ya asilimia 70 wana matatizo ya mtoto wa jicho huku asimilia 20 wanakabiliana na shinizo la damu la macho  jambo ambalo limekuwa likiwapa wakati mgumu  katika kutekeleza majukumu yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana Mratibu wa Macho Wilaya ya Muheza, Sista Adelina Swai wakati wa zoezi la upasuaji wa macho kwa wakazi wa wilaya hiyo wenye matitizo ya mtoto wa jicho yaliyofanyika kwenye kituo cha Afya Ubwari lililokuwa likiendeshwa na Taasisi ya Medewell Charitable Health Centre.

Alisema uwiano wa asilimia za matatizo hayo ya macho umekuwa mkubwa kutokana na uchunguzi ambao wamekuwa wakiufanya kwenye maeneo ya vijiji mbalimbali wilayani humo

Alisema wamegundua suala hilo baada ya kufanya uchunguzi kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ikiwemo kuwapima macho ili kuweza kuwabaini na hatimaye kuweza kupatiwa matibabu na taasisi hiyo ya medewell kwa

“Nawashukuru sana taasisi ya Medewell kwa msaada mkubwa wa kufanya upasuaji wa macho kwa wananchi wenye matatizo hayo kwani suala hili lilikuwa tatizo kubwa kwa jamii hivyo tunaimani watashiriki kwenye shughuli za kujiletea kimaendeleo,” alisema

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ubwari, Dk. Raymond Mhina, alisema upasuaji huo umefanywa kwa wananchi 58 waliofika kwenye kituo hicho cha Afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Niwashukuru sana taasisi hiyo kwa kuendesha shughuli za upasuaji kwenye kituo hiki jambo ambalo limesaidia kuwaondolewa changamoto cha maji wananchi,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles