32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ufaransa yapitisha kodi kampuni za kidigitali licha ya kitisho cha Marekani

WASHINGTON –MAREKANI

UFARANSA imepitisha kodi kwenye kampuni na vifaa vya kidigitali pamoja na vitisho vya kisasi toka Marekani ambayo ilionyesha wasiwasi mkubwa kwamba kampuni zake zitawekewa kodi isiyostahili.

Ufaransa imeamua kuwa asilimia tatu ya kodi itatozwa nchini humo katika mauzo yanayotokana na kampuni za kimataifa kama Google na Facebook.

Pia imesema kampuni kama hizo za Ufaransa zenye makao makuu nje ya nchi hiyo zitalipa kidogo au hazitolipa kabisa.

Ufaransa pia imeamua kuwa kampuni yeyote ya kidigitali yenye mapato ya zaidi ya Euro milioni 670 au Dola milioni 850 – ambayo angalau Euro milioni 25 inazalisha Ufaransa –zitatakiwa kulipa kodi.

Tume ya Ulaya inakadiria kuwa kodi inayopaswa kutozwa kwa wastani wa biashara za ndani ya umoja huo ni ile ya asilimia 23 za faida zao, wakati kampuni za intaneti zinalipa asilimia nane au tisa tu.

Kabla ya uamuzi huo wa Ufaransa, Rais wa Marekani Donald Trump aliagiza kufanyika uchunguzi wa kodi ya kidigitali iliyopangwa kutozwa nchini Ufaransa.

Mwakilishi wa Marekani katika masuala ya biashara, Robert Lighthizer, alisema kuwa Marekani ina wasiwasi mkubwa kwamba kampuni  zake zitawekewa kodi kubwa hali ambayo itaathiri.

Wiki iliyopita Bunge la taifa nchini Ufaransa liliidhinisha sheria hiyo ya kodi ya kidigitali.

Kampuni ambazo zilionekana kuwa zitaathirika na sheria hiyo ni pamoja na zile za Marekani kama Google, Amazon na Facebook.

Hatua ya Marekani kuitishia Ufaransa juu ya jambo hilo ni mwendelezo wa hatua kama hizo nyingine za kuendelea kujilinda kibiashara.

Itakumbukwa ni hivi karibuni tu Marekani na China  zimekubalina kuanza mazungumzo ya kibiashara baada yale ya mwezi Mei kukwamba na hivyo kusababisha uchumi wa dunia kusuasua.

Rais wa Marekani, Trump na Rais wa China, Xi Jinping  walifikia makubliano hayo katika mkutano uliokutanisha mataifa tajiri duniani maarufu kama -G20  uliofanyika nchini Japan wiki chache zilizopita.

Trump pia alisema ataruhusu kampuni za Marekani kuendelea kununua au kuuza kwenye kampuni kubwa ya teknolojia ya China ya Huawei.

Kabla ya mkutano huo Trump alitishia kuongeza dola bilioni 300 za kodi kwenye bidhaa zinazotoka China.

Baada ya kukutana na Rais Xi, kiongozi huyo wa Marekani alisema hataongeza kodi nyingine na kwamba ataendelea kuzungumza na China.

Trump pia alisisitiza katika mkutano na waandishi wa habari kwamba kampuni za teknolojia za Marekani zitaweza kununua kwa kampuni ya Huawei ya China kama kawaida na hivyo kuondoa marufuku iliyowekwa mwezi uliopita na kitengo cha biashara cha Marekani.

Marufuku hiyo ilikuwa inazuia kampuni za teknolojia za Marekani kununua ya vifaa kutoka  Huawei, kwa kile alichoeleza kuwa ilikuwa ikitishia usalama wa nchi yao.

Mataifa hayo mawili yenye nguvu ya kiuchumi duniani, Marekani na China walikuwa wakipambana kwenye vita ya kibiashara kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Trump  alikuwa akiishutumu China kuiiba utalaamu wake na kulazimisha kampuni za Marekani kutumia pamoja siri za kibiashara ili kufanya biashara na China.

China iliijibu Marekani ikisema taifa hilo linataka kufanya mabadiliko yasiyo na sababu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles