25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ufaransa ‘yafukuzwa’ Libya

TRIPOLI, LIBYA

MAELFU ya wananchi nchini Libya wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njano kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya Serikali ya Rais Emmanuel Macron dhidi ya nchi yao.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, washiriki wa maandamano hayo wamelaani vikali operesheni za Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi linalojiita ‘Jeshi la Kitaifa la Libya’ pamoja na uungaji mkono wa kijeshi wa Ufaransa dhidi ya nchi yao. 

“Sisi wazawa wa Tripoli kama walivyo wakazi wa miji mingine ya Libya, tumekuja hapa kuonyesha upinzani wetu kwa utawala wa mtutu wa bunduki wa Haftar na mashambulizi yake,” amesema mmoja wa waandamanaji.

Siku chache zilizopita, Shirika la Habari la Al Jazeera liliripoti kwamba, meli ndogo ya kivita mali ya Ufaransa ilituma silaha na zana za kijeshi kwa wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, boti ndogo za mwendo kasi zilitumika kupakua shehena ya silaha kutoka kwenye meli hiyo ya kivita ya Ufaransa. 

Aidha wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Abdelkrim Zbidi alinukuliwa akisema kuwa maofisa wa usalama wa nchi hiyo waliwatia mbaroni watu 13 wakiwa na pasi za kusafiria za Ufaransa kwenye kivuko cha Ra’s Ajdir katika mpaka wa Libya. 

Wiki iliyopita, Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya ilitangaza kukata ushirikiano wake wa kiusalama na serikali ya Ufaransa kutokana na hatua ya nchi hiyo kuliunga mkono kundi la wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar. 

Wapiganaji wa kundi hilo walianzisha mashambulizi makali Aprili 4 mwaka huu, dhidi ya mji wa Tripoli sambamba na kushambulia makao makuu ya Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa mjini humo. Hujuma hizo hadi sasa zimepelekea karibu watu 270 kuuawa na wengine 1300 kujeruhiwa, sambamba na watu 35,000 kuwa wakimbizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles