Na Hassan Daudi, Mtanzania Digital
01. Hatua ya makundi ilikuwa na mabao ya kufunga 94 katika mechi 36. Kasi ya upasiaji nyavu imepanga, ukilinganisha na fainali zilizopita za mwaka 2016, ambapo ni mabao 69 tu yaliyofungwa.
02. Wakali wa kuzifumania nyavu hawakubaki nyuma msimu huu kwani mechi za makundi zilishuhudia mabao nane ya kujifunga.
03. Asilimia 63 ya mabao yalipatikana kipindi cha pili. 04. Hakuna aliyevunja rekodi ya nyota wa Urusi, Dmitri Karachenko, akiwa ndiye mchezaji aliyefunga bao la mapema zaidi (dk. moja na sek. saba) kwenye historia ya Euro.
05. Italia, Ubelgiji na Uholanzi ndizo timu pekee zilizomaliza hatua ya makundi pasi na kufungwa wala sare.
06. Robert Lewandowski ndiye mchezaji aliyefumua mashuti mengi hatua ya makundi (12), akiwazidi moja Cristiano Ronaldo na Memphis Depay.
07. Pierre-Emile Hojbjerg (Denmark) na Steven Zuber (Uswis) ndiyo waliiongoza kwa ‘asisti’, kila mmoja akiwa na tatu. 08. Kipa wa Uturuki, Ugurcan Cakir, ndiye aliyeongoza kwa idadi kubwa (18) ya hatari alizookoa, akifuatiwa na Danny Ward wa Wales (14).
09. Cristiano Ronaldo ndiye anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa na mabao matano.