Raia wa Finland wanapiga kura katika uchaguzi wa bunge ambapo masuala muhimu kama ustawi wa taifa na mabadiliko ya tabianchi ndiyo yaliyopewa kipaumbele.
Kulingana na utafiti wa kura ya maoni ya raia Chama cha Social Democratic cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto kinaungwa mkono kwa asilimia 19.
Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia hata hivyo kinashika nafasi ya pili kwa uungwaji mkono wa asilimia 16. Asilimia 36 ya raia tayari wameshapiga kura ya awali.
Kuna vyama vya kisiasa 19 na wabunge 2,500 wanaogombania viti 200 bungeni.