29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

UN yaitaka Sudan idumishe amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anaendelea kufuatilia hali ya Sudan kwa karibu huku akisisitiza kudumishwa amani na utulivu.

Guterres akumbushia wito wake na matarajio yake kwamba matakwa ya kidemokrasia ya watu wa Sudan yatafikiwa kupitia mchakato unaofaa , wa kisiasa na jumuishi.

Halikadhalika Guterres amewahakikishia watu wa Sudan utayari wa Umoja wa Mataifa kusaidia nchi hiyo katika siku zijazo.

Serikali ya rais wa Sudan Omar al-Bashir imepinduliwa na sasa inashikiliwa na jeshi kwa kipindi cha miaka miwili.

Omar al-Bashir amekuwa kwenye utawala tangu mwaka 1989 baada ya mapinduzi na kuchaguliwa rasmi rais wa nchi hiyo 1993.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles