24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ubunifu wa UDOM wamkosha Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa, amevutiwa na ubunifu uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu. 

Waziri Mkuu Kssim Majaliwa, akieleza jambo wakati wa akiwa kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Elimu yaliyofanyika mkoani Tanga. 

Akizungumza wakati alipotembelea Banda la UDOM katika Kilele cha Maadhimisho hayo Ijumaa Mei 31, 2024, Majaliwa amekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuweza kubuni vifungashio mbadala ambavyo ni rafiki kwa Mazingira, na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana. 

Aidha, ametoa wito kwa UDOM kuendelea kufanya tafiti na kuja na bunifu nyingi za kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, likiwemo suala la vijana kujiajiri. Naye, mbunifu wa vifungashio hivyo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma ambaye ni Mkufunzi Msaidizi, Mohammed Amini, kutoka Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati amesema vifungashio hivyo vinatengenezwa kwa malighafi taka na zao la mwani na hivyo gharama za kuzalisha ni ndogo kiasi cha kila mwananchi kuzimudu, na pia ni bidhaa rafiki katika kutunza mazingira.

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu mkoani Tanga. Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na maonesho ya Elimu, Ubunifu na Teknolojia. 

Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yalianza tarehe 25 Mei na kufungwa Mei 31, 2024, yakiwa yamefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Tanga, yakihusisha wadau wote wa Elimu nchini vikiwemo Vyuo Vikuu, Vyuo vya Kati, Taasisi na Mashirika ya Elimu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles