26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Ubelgiji kusaidia wapinga adhabu ya kifo

Na SABINA WANDIBA Na LILIAN SANGA-DAR ES SALAAM

UBALOZI wa Ubelgiji nchini Tanzania, umeahidi kusaidia kuziwezesha taasisi zitakachokuwa tayari kupaza sauti zao kupinga adhabu ya kifo duniani.

Akizungumza katika siku ya maadhimisho ya 18 ya kupinga adhabu ya kifo duniani, Balozi wa Ubelgiji nchini, Peter Van Acker amesema kuwa, Serikali ya Ubelgiji inaungana na mataifa mengine duniani kupinga adhabu ya kifo.

Alisema kuwa, katika kuunga mkono adhabu hiyo, serikali yake inajitolea kuziwezesha taasisi zote zitakazojitokeza kupinga adhabu hiyo inayokatisha maisha ya binadamu.

“Ni miaka mingi sasa imepita nchi ya Ubelgiji haijatoa hukumu ya kifo kwa mtu yoyote japo sheria hiyo bado ipo, ni ngumu sana kutekeleza hii adhabu kwa kuwa inakatisha maisha ya binadamu,” alisema Balozi huyo.

Aidha aliongeza kuwa, katika nchi hiyo kuna mashirika na taasisi nyingi zinazopaza sauti kupinga adhabu ya kifo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga alisema kuwa, siku hiyo ni muhimu kwa kituo chao kuungana na Mataifa mengine duniani kupinga adhabu ya kifo.

Wanaiomba serikali kufuta adhabu ya kifo kwakuwa haionyeshi kubadilisha jamii na kuifanya kuachana na makosa ya mauaji.

“Pamoja na kuwepo adhabu ya kifo lakini bado matukio ya mauaji yanaongezeka siku hadi siku, tunamshukuru rais Magufuli kukataa kusaini adhabu hiyo na kutoa msamaha kwa wafungwa waliokuwepo gerezani kwa muda mrefu,” alisema Wakili Henga.

Mkurugenzi wa Chama cha Elimu kwa Watoto  (CHESO) Richard Shilamba alisema kuwa, taasisi hiyo inasaidia watoto walioathirika kisaikolojia baada ya wazazi wao kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji ama dawa za kulevya.

“Waathirika wakubwa wa adhabu hii ni watoto ambao wazazi wao wamehukumiwa kifo, wengi wanakosa haki ya kupata elimu bora na wengine wanaathirika kisaikolojia, baadhi tunawasaidia kuwasomesha kwakuwa wanakosa msaada kielimu,” alisema Shilamba.

Alisema, ni vyema serikali ikafuta adhabu hiyo ya kifo na kuweka adhabu mbadala ili kutoa haki ya kuishi kwa binadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles