30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tutapitia mifumo yote ya usambazaji pembejeo-Prof. Mkenda

Na Derick Milton, Simiyu.

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara yake kwa sasa inafanya mapitia makubwa ya mifumo mizima ya kitaasisi ambayo imekuwa ikitumika katika ugawaji wa pembejeo za kilimo hasa zao la pamba.

Prof. Mkenda amesema hayo leo, Jumanne Desemba 15, wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika mjini Bariadi, ambapo amesema kumekuwepo mengi ya wakulima kupata pembejeo kwa muda muafaka.

Kabla ya kuzungumza kwenye kikao hicho Prof. Mkenda, alipokea malalamiko ya baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wakuu wa wilaya, wabunge, wenyeviti wa halmashauri juu ya kutokuwepo kwa mbegu za kutosha kwa wakulima.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi amesema kuwa kuna changamoto upungufu wa mbegu za kutosha kwa wananchi wao, na wananchi kulalamika mara kwa mara juu ya kukosa mbegu.

Kilangi amesema kuwa tatizo la mbegu limekuwepo kila mwaka, pamoja na viuatilifu, ambapo ameiomba serikali kuangalia upya mfumo ambao bodi ya pamba imekuwa ikitumia katika kugawa pembejeo hizo.

Mara baada ya kuwasilisha changamoto hizo, Prof. Mkenda amesema kuwa amewaagiza wataalamu wa wizara hiyo kufanya uchambuzi wa mifumo hiyo ili iweze kupitiwa upya na kuboresha sekta ya kilimo.

“Nimekutana na malalamiko mengi sana juu ya usambazaji wa mbolea, mbegu na viuatilifu, kama wizara tunapitia upya mifumo hiyo, hasa kwenye zao la pamba ambalo wakulima wengi wamekuwa wakilalamika,” amesema Prof. Mkenda.

Aidha Waziri huyo ameongeza kuwa Wizara yake itafanya uchunguzi wa viuatilifu vyote ambavyo vimekuwa vikiletwa nchini kutoka nje ya nchi kwa ajili ya matumzi ya visumbufu vya mazao kwani wakulima wamekuwa wakilalamika kutokuwa na ubora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles