23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tusiwakomoe Waandishi wa Habari- Meena

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), NEVILLE Meema amesema baadhi ya vipengele vya Sheria ya Habari ya Mwaka 2016, vinailazimisha mahakama kutenda kwa matakwa ya watungaji wa sheria hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 29, 2022, wakati akizungumza katika Kipindi cha Sun Down kinachorushwa na Radio Ukweli (Ukweli FM), Mjini Mrorogoro.

“Tusitunge sheria kwa ajali ya kuilazimisha mahakama kutenda kwa mujibu wa yaliyopo mioyoni mwa watunga sheria,” amesema Meena.

Akifafanua kauli yake amasema, hatua ya sheria kumuelekeza hakimu kutoa kifungo kisichopungua miaka mitatu, ni kumlazimisha asitoe hukumu chini ya kiwango hicho.

“Inawezekana hakimu akaona kosa la mwandishi linahitaji kifungo cha miaka miwili au mmoja au miezi sita na pengine miezi mitatu ama kifungo cha nje.

“Lakini kutokana na sheria hii, hakimu hawezi kutoa kifungo nje ya kile kilichoelezwa na sheria, sasa huku ni kulazimisha kila aliyetenda kosa kwenye tasnia ya habari afungwe sio chini ya miaka mitatu. Jambo hili tunaona lina ukakasi,” amesema Meena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles