28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tumieni bidhaa za ndani kuimarisha viwanda- Mwijage

Charles Mwijage
Charles Mwijage

Na FEDINANDA MBAMILLA,DAR ES SALAAM

WATANZANIA wameshauriwa kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ili kukuza biashara na kuunga mkono juhudi za Serikali za kutaka kujenga nchi ya viwanda.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, katika ziara yake ya kukagua kiwanda cha Milkcom Dairies Limited kilichopo Kibada wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam.

“Tukipenda bidhaa zetu tunatengeneza soko kwa viwanda vyetu kuzalisha zaidi, kukua na kujenga uchumi wetu,” alisema.

Alisifu juhudi zinazofanywa na kiwanda hicho kinachozalisha maziwa kwa jina la Dar Fresh na bidhaa nyingine za maziwa na maji ya chupa.

Kiwanda hicho kiko katika harakati za kuanza kuzalisha vinywaji baridi na kukamua matunda kwa ajili ya kutengeneza juisi mbalimbali.

“Nimefurahishwa na kazi yenu, mnafanya vizuri,” alisema.

Kiwanda hicho chenye ng’ombe wa maziwa 3,000, kinazalisha wastani wa lita 10,000 za maziwa kila siku.

Pamoja na hali hiyo, pia kinakusanya maziwa toka kwa wafugaji hasa katika maeneo ya mikoa ya Morogoro na Pwani.

Akitoa maelezo kwa Waziri Mwijage,  Mkurugenzi wa Maziwa ya Dar Fresh, Yusuph Said, alisema utaratibu huo umesaidia kutengeneza soko la uhakika kwa wafugaji hao.

“Tunakusanya wastani wa lita 8,000 kila baada ya siku moja kutoka kwa wakulima hao,” alisema Said.

Waziri aliuahidi uongozi wa kiwanda hicho kufuatilia kwa karibu ili kupata umeme wa uhakika kutoka gridi ya taifa na miundombinu mingine ya muhimu ili waweze kuwa washindani zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles