27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

TUJIPANGE KUKABILI CHANGAMOTO MPYA KATIKA ELIMU

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


MUHULA mpya wa masomo unatarajiwa kuanza wiki ijayo ambapo wanafunzi wengi wakiwamo wa darasa la kwanza na wale wanaopanda darasa wana shauku kubwa ya kwenda shule.

Kila mwaka kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa kuanza darasa la kwanza ambalo kwa kiasi kikubwa limechangiwa na maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanywa.

Baadhi ya maboresho hayo yanatokana na uwepo wa Sera ya Elimu ya mwaka 2014.

Mathalani utoaji wa elimu bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne ni mojawapo ya mambo yaliyopendekezwa katika sera hiyo ambayo nayo yamechangia kuwapo kwa ongezeko hilo.

Sera hiyo pia ilipendekeza kuwapo kwa maboresho ya muundo wa elimu ili kupunguza miaka ya kupata elimu ya awali na kupunguza umri wa kuanza

darasa la kwanza.

Kwa mujibu wa sera hiyo, muundo wa elimu wa sasa wa 2+7+4+2+3+ pamoja na kwamba ulionekana kuwa umelisaidia Taifa hadi tulipofikia lakini huchukua muda mrefu tangu mwanafunzi anapoanza elimu ya msingi mpaka anapohitimu chuo kikuu.

 

Hivyo ilipendekezwa kuwa na muundo wa 1+6+4+2+3+ ambao mhitimu atamaliza mzunguko wa masomo kwa muda mfupi na mikondo ya ufundi ijumuishwe kwenye elimu ya msingi na sekondari.

 

Kama hili litatekelezwa ni wazi kuwa kutasababisha ongezeko maradufu la wanafunzi wenye umri wa kuanza darasa la kwanza hivyo kutakuwa na uhitaji mkubwa wa walimu, miundombinu ya madarasa na vyoo, madawati, vitabu na vitendea kazi vingine.

Kuwapo kwa ongezeko hilo ni dhahiri kwamba walimu waliopo kazini hawatakidhi mahitaji ya shule zote kutokana na ukweli kwamba hata kabla ya kusajiliwa kwa wanafunzi hao wapya mahitaji ya walimu tayari ni makubwa.

Hivyo inahitajika nguvu ya ziada kukabiliana na changamoto hizo. Si rahisi kwa Serikali pekee kumudu mzigo huu mkubwa bali kwa kuunganisha nguvu ya pamoja baina ya Serikali, wadau na wananchi ili kupata vyumba vya madarasa vya kutosha na mahitaji mengine.

Kuwepo na msukumo kwa serikali za mitaa na wadau kuona kuwa wanao wajibu wa kuchangia katika elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles