25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TUGHE YAPOTEZA WANACHAMA 9,000 UHAKIKI WAFANYAKAZI HEWA

Kuondolewa kwenye ajira kwa wafanyakazi hewa na wale wa darasa la saba imesababisha Chama  cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe)  kupoteza  zaidi ya wanachama 9,000.

Hatua hiyo imesababisha kupungua kwa mitaji na wanachama hali inayowalazimu kuangalia namna ya kupata wanachama wapya hususani wale wanaoanza kuajiriwa serikalini.

Katibu Mtendaji wa Tughe, Eliabert Mkunda amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa Baraza Kuu Tughe Taifa kilichofanyika mjini Morogoro jana.

Mkunda amesema baada ya kuathiriwa na zoezi hilo chama hicho sasa kinafanya kinafanya jitihada nyingine za kupata wanachama wapya hasa ambao wanaajiriwa kwa sasa na serikali  ili kuongeza wanachama.

Awali akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa chama hicho, Hashim Mntambo amesema pamoja na mambo mengine wanaidai Serikali Sh milioni 480 ambapo fedha hizo zimeshahakikiwa kuwa deni halali lakini bado serikali haijawalipa.

“Kucheleweshwa kwa fedha hizo  kunachangia  kuyumbisha  uendeshaji wa chama na kushindwa kufikia malengo yake kwa muda muafaka kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa za chama,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles