26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, November 2, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP, PUTIN KUKUTANA MARA YA PILI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani, Donald Trump ambaye anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu mkutano wake wa kilele na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, mjini Helsinki wiki hii, amesema anakusudia kumwalika kiongozi huyo katika mkutano mwingine tena baadaye mwaka huu na tayari mazungumzo yanaendelea.

Licha ya Rais Donald Trump kukumbwa na ukosoaji mkubwa baada ya mkutano wa kilele kati yake na Rais Vladimir Putin, wiki hii kuhusu kile kilichotazamwa kuwa kuukubali msimamo wa Putin kwamba Urusi haikuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016, msimamo ambao ni kinyume na msimamo wa mashirika ya ujasusi ya Marekani, msemaji wa Ikulu ya White House, Sarah Sanders, amesema kwenye ukurasa wa Twitter kuwa, mkutano kati ya Trump na Putin huenda ukafanyika baadaye mwaka huu mjini Washington.

Sanders amesema Rais Trump amemwambia mshauri wake wa usalama wa taifa, John Bolton, kumwalika Rais Putin, mjini Washington na tayari mazungumzo kuhusu mwaliko huo yameshaanza.

Mwaliko huo umemshangaza kwa mkurugenzi wa ujasusi wa Marekani, Dan Coats, wakati akihojiwa moja kwa moja katika kongamano la usalama la Aspen Jimbo la Colorado.

Akizungumzia mkutano uliopita kati ya Trump na Putin, Coats alisema: “Sijui kilichojiri katika mkutano huo. Ninafikiri kadiri muda unavyosonga na tayari rais amedokeza baadhi ya yale yaliyojiri. Ninafikiri tutafahamu mengi. Lakini hilo ni jukumu la rais. Lau angaliniuliza namna lilivyopaswa au kulishughulikia, ningelipendekeza njia tofauti. Lakini hilo si jukumu langu, wala kazi yangu na ndivyo hali ilivyo.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles