LONDON, Uingereza
RAIS wa Marekani, Donald Trump amemkosoa vikali Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa kusema Muungano wa Kujihamani wa Mataifa ya Ulaya (Nato) ni “ubongo uliyokufa”.
Rais Trump ambaye yuko nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa muungano wa kujihami kwa mataifa ya magharibi, Nato unaoadhimisha miaka 70 tangu ulipobuniwa.
Akiwa katika mkutano na wanahabari, Trump alisema Nato, inajukumu muhimu na matamshi ya Rais l Macron ni “matusi”.
Alisema anaona Ufaransa ikijiondoa kutoka Nato, lakini hakuelezea sababu zake.
Nato – muungano wa kujihami kwa mataifa ya magharibi uliundwa, baada ya vita vikuu vya pili vya dunia kukabaliana na kitisho cha uwezekano wa kuendelea kutanuka kwa muungano wa Usoviet.
Rais Macron alielezea muungano huo kama “ubongo uliokufa”, akisisitiza kile anachokiona kama kutokuwa na utashi wa mdhamini mkuu wa Marekani.
Mkutano huo, ulitajarajiwa kuanza tayari umekumbwa na mzozo mkali kati ya wanachama wake Ufaransa na Uturuki, na muendelezo wa suala la mchango wa mataifa mwanachama.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, alisema atapinga mpango wa umoja huo wa kiulinzi kwa nchi za Baltiki iwapo haitaiunga mkono Uturuki katika vita vyake dhidi ya kikundi cha Kikurdi ambacho inakichukulia kama cha kigaidi.
Akiwa ameketi karibu na Katibu Mkuu wa Nato, Jens Stoltenberg, Rais Trump alisema muungano wa Nato, “una jukumu muhimu”, lakini pia alipoulizwa mtazamo wake kuhusiana na matamshi ya Bwana Macron.
Trump alijibu akisema kiongozi wa Ufaransa, “amezikosea heshima” nchi zengine mataifa wanachama.
“Matamshi yake ni machafu. Nadhani Ufaransa ina kiwango kikubwa cha ukosefu wa kazi. Uchumi wa Ufaransa wenyewe hauko vizuri, “alisema.
“Ni matamshi makali kwa mtu kuyazungumza, huku Ufaransa ikiwa inapitia kipindi kigumu kama hichi hasa ukizingatia kile kinachoendelea. Mwaka huu wamekuwa na wakati mgumu kweli. Huwezi kuanza kuzunguka huku na kule, ukisema matamshi kama haya kuhusu Nato. Huu ni ukesofu heshima wa hali ya juu.
“Kwa wakati huu hakuna anayehitaji usaidizi wa Nato kama Ufaransa…manufaa inayopata Marekani ni machache mno. Huu ni usemi hatari,”alisema
Pia alirejea malalamishi yake ya muda mrefu kwamba mataifa mengine wanachama wa muungano wa Nato, hawachangii kama inavyohitajika kipesa na kuitaja Ujerumani kama mfano.
Lakini kulingana na mazungumzo ya Rais Macron mwezi uliopita, alilalamikia ukosefu wa wanachama wa Nato kwamba hawatoi tena ushirikiano katika masuala muhimu.
Mwezi uliopita, rais wa Ufaransa aliitaja Nato kuwa muungano ”usio na maana”, akisema kuwa wanachama wake hawashirikiani kuhusu masuala muhimu.
Trump aliwasili nchini Uingereza juzi usiku kabla ya hafla maalumu itakayoandaliwa na malkia katika kasri la Buckingham Palace.
Pia anajiandaa kufanya mazungumzo ya pembeni na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na katibu mkuu wa Nato.
Hali ya taharuki imekuwa ikipanda tangu Rais Trump, alipolalamika mara kadhaa kuwa mchango wa mataifa ya Ulaya ambayo ni wanachama haukidhi mahitaji ya shirika hilo ambalo lilibuniwa kukabiliana na vitisho baada ya vita vikuu vya pili vya dunia ili kupanuka kwa ukomyunisti baada ya vita vya pili vya dunia.
Nato inakadiria kuwa kufikia mwaka 2019 ni mataifa manane miongoni mwao Marekani ndio yalioafikia viwango vya mchango uliowekwa kama ilivyokubaliwa na mataifa wanachama.