32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Trump atumia kura ya turufu kuilinda Saudia

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump ametumia kura ya turufu kupinga azimio la Bunge la nchi yake linaloitaka Marekani iache kuisaidia Saudi Arabia katika vita ya Yemen.

Hata hivyo, Spika Nancy Pelosi amesema kura ya turufu ya Rais Trump itaendeleza aibu ya Marekani ya kuhusika na mgogoro wa Yemen.

Trump alitumia kura hiyo juzi kuzuia azimio la Bunge lenye lengo la kukomesha msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Saudi Arabia. Azimio hilo liliungwa mkono na Baraza la Wawakilishi pamoja na lile la Seneti. Hii ni mara ya pili kwa Trump kutumia kura ya turufu kupinga azimio la Bunge.

  Na ili kuibatilisha kura ya Rais, theluthi mbili ya wabunge itahitajika jambo ambalo kwa sasa haliwezekani katika Bunge lililogawanyika kwa kiasi kikubwa baina ya chama tawala cha Republican na Democratic.

Kwa kuipinga sera ya mambo ya nje ya Rais Trump, Chama cha Democtratic siku ya Jumatatu kilipitisha azimio la kuutaka utawala wa Trump kusitisha kuiunga mkono Saudi Arabia katika vita ya Yemen.

Pelosi aliwaambia waandishi wa habari kwamba kutiwa saini muswada huo ni kutekeleza wajibu wa Bunge katika kusimamia matumizi ya kijeshi. Kupitishwa kwa azimio hilo na pande zote mbili za Bunge kulizingatiwa kuwa hatua ya kihistoria, kwa  sababu hii ni mara ya kwanza kwa muswada wa Bunge wa kupinga vita kuwasilishwa kwa Rais kwa mujibu wa sheria inayohusu vita iliyopitishwa  mwaka 1973.

Hata hivyo, uamuzi wa Trump si wa kushangaza, kwani amekuwa akiiunga mkono Saudi Arabia kwa nguvu hata baada ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi kuuawa na idara za ujasusi za Marekani kubainisha mrithi wa mfalme wa Saudi Arabia Mohammed alihusika na mauaji hayo.

Akitetea uamuzi wake, Trump alisema azimio hilo la wabunge halikuwa la lazima. Alisema azimio hilo ni juhudi za hatari za kudhoofisha mamlaka yake ya kikatiba, hatua ambayo ameeleza inahatarisha maisha ya raia wa Marekani pamoja na ya wanajeshi jasiri wa nchi hiyo.

Trump pia alidai azimio la Bunge lingeathiri sera ya nje ya Marekani na kuathiri uhusiano wa Marekani na Saudi Arabia. Alieleza kwamba mazungumzo yatahitajika ili kuleta amani nchini Yemen na amesisitiza kuwa Marekani haihusiki na mapigano moja kwa moja nchini Yemen ukiondoa vita dhidi ya magaidi wa Al-Qaeda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles