24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Afreximbank kusimamia mradi wa madini Sierra Leone

FREETOWN, SIERRA LEONE

BENKI ya African Export-Import (Afreximbank) imekabidhiwa mamlaka ya kuwa mshauri wa ujumuishi wa kifedha na mpangaji mkuu wa mradi wa mgodi wa bauxite wenye thamani ya dola milioni 130 nchini hapa.

Imekabidhiwa mamlaka hayo na Kampuni ya Sierra Mineral Holdings 1 Limited (Vimetco).

Mamlaka hayo yalitangazwa mjini hapa wiki iliyopita wakati wa kikao cha kazi kilichoandaliwana Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio.

Wengine walioshiriki ni wawakilishi wa Vimetco, mfadhili mkuu wa mradi VI Holdings, kampuni mama ya Vimetco na Afreximbank.

Chini ya masharti ya mamlaka hayo, kama yalivyoelezwa katika barua ya makubaliano uliosainiwa kati ya Vimetco na Afreximbank wakati wa kikao cha kazi na Rais Bio, Afreximbank itakuwa na jukumu kuu la kutoa ushauri wa kifedha na namna ya kutumia mtaji kwa ajili ya mradi huo.

Sherehe za kusaini mkataba ziliambatana na uzinduzi rasmi wa upanuzi wa mradi huo, ambao utashuhudia ujenzi wa mgodi mpya kuanzia mwaka 2020, huku uzalishaji ukitarajia kuanza katikati ya mwaka 2022.

Mgodi wa bauxite wa Vimetco utazalisha madini ya aluminium na alumina tri-hydrate, ambayo hutumika katika viwanda vya vitu vya kuhifadhi joto na keramik kama vile vigae pamoja na kusafishia maji na kadhalika.

Ujenzi wa mgodi mpya wenye teknolojia ya kisasa utakuwa wa kwanza kwa Sierra Leone linapokuja suala la maendeleo ya sekta ya madini. Mradi huo utazalisha ajira na kupelekea maendeleo ya miundombinu kupitia ujenzi wa shule, hospitali, barabara, madaraja na mengineyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles