25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TRUMP APENDEKEZA ADHABU YA KIFO KWA WAUZA DAWA ZA KELEVYA


NEW HAMPSHIRE, MAREKANI

RAIS Donald Trump amesema anataka kuweka adhabu kali ikiwemo ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Hatua hiyo alisema ni kwa lengo la kukabiliana na ongezeko kubwa la watumiaji dawa hizo ndani ya Marekani.

Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa hapa, alisema wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa, wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo alisema haridhishwi nalo.

Aliongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara na kutenga fedha.

“Mwezi Oktoba mwaka jana tulitangaza tatizo hili kama janga la dharura kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita.

“Tumelifanyia kazi na Bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola bilioni sita katika bajeti mpya ya mwaka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili,” alisema.

Hata hivyo, Trump alielezea mikakati iliyowekwa katika kukabiliana na dawa za kulevya hadi sasa, ambayo inalenga kupunguza kiasi cha uhitaji wa dawa hizo na idadi ya wanaojiingiza kuzitumia.

Trump pia aliahidi kujenga taifa huru katika masuala ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kizazi kijacho na kuhakikisha hakuna mazingira yatakayosababisha watu kujitumbukiza katika kilevi hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles