25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Trump aja na mkataba mpya wa nyuklia

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump amesema anataka mkataba mpya wa nyuklia usainiwe na Urusi na China kwa pamoja.

Trump amesema amekuwa akizungumza na na nchi hizo mbili kuhusu wazo hilo na wote “walilifurahia sana sana”.

Kauli hiyo ya Trump inakuja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba muhimu wa nyuklia na Urusi, ikieleza  kukasirishwa na aina mpya ya silaha zake.

Juzi Marekani ilijitoa kwenye mkataba  unapiga marufuku zana za mafasa ya kati (INF) kwa sababu ya hatua hiyo ya Urusi.

Mkataba huo ulisainiwa na Rais wa Marekani, Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mwaka 1987.

Mkataba huo (INF) ulipiga marufuku matumizi ya zana za masafa ya kati yanayopiga kilomita 500 hadi 5,500 (310-3,400 miles).

Kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba huo Ijumaa kumefuatia shutuma za Marekani kwamba Urusi ilikuwa imekiuka mkataba huo kwa kuunda mtambo mpya wa mfumo makombora kauli ambayo inapingwa vikali na Urusi.

Akijibu maswali juu ya ni vipi ataepuka silaha za nyuklia kufuatia kuvunjika kwa mkataba wa INF , Trump alisema utawala wake umekuwa ukizungumza na Urusi kuhusu mkataba wa nyuklia, ili waachane na baadhi ya silaha.

“Tutahitaji kwa vyovyote vile kuijumuisha Uchina wakati fulani ,”aliongeza.

Trump amesema mkataba wa aina hiyo unaweza kuwa kitu cha kizuri kwa dunia na kwamba anaamini hili litatekelezwa.

“Uchina ilifurahia sana, sana kuhusu kuzungumzia juu ya suala hili na ilikuwa hivyo hivyo kwa Urusi . Kwa hiyo ninadhani tutakuwa na mkataba wakati fulani “, Trump aliwambia waandishi wa habari

Marekani inataka kuchukua uamuzi wa kuja na mkataba mpya katika wakati ambao Urus inadaiwa kumiliki aina mpya ya silaha, kwa kutengeneza makombora kadhaa ya 9M729 – yanayojulikana na Nato kama SSC-8.

Shutuma hizi pia ziliwasilishwa kwa washirika wa Marekani katika muungano wa Nato, ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani.

“Urusi inawajibika kwa kuvunjika kwa mkataba”, alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo katika taarifa aliyoitoa Ijumaa.

“Kwa uungaji mkono kamili wa washirika wetu wa Nato, Marekani imeamua kuwa Urusi ndio imesababisha kuvunja mkataba, imekuwa ikikiuka mara kwa mara wajibu wake chini ya mkataba ,”aliongeza.

Mwaka 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kuwa mkataba huo haushughulikii maslahi ya Urusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles