25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yakusanya trilioni 11.9 kwa miezi tisa

KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kukusanya Sh trilioni 11.96 kuanzia Julai 2018 hadi Machi 2019.

Akizungumza  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa 2018/19, Januari walikusanya Sh trilioni 1.30 Februai walikusanya Sh trilioni 1.23 na Machi Sh trilioni 1.43.

Alisema katika nusu ya mwaka wa fedha 2018/19 kati ya Julai hadi Desemba 2018 TRA ilikusanya Sh trilioni 7.99 ambayo ukuaji wake katika makusanyo ya mwaka uliopita kwa kipindi kama hicho ulikuwa ni asilimia 2.01.

“Katika kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea, mamlaka ya mapato imekuwa ikitoa elimu mbalimbali kuhusu masuala ya kodi  kuwahamasisha walipakodi kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya nchi,” alisema Kayombo.

Alisema   Julai 2018 walifanikiwa kukusanya Sh trilioni 1.20 huku  Agosti wakikusanya Sh  trilioni 1.27 na Septemba Sh  trilioni 1.36.

Aliongeza kuwa  Desemba walifanikiwa kukusanya Sh  trilioni 1.63, huku  Novemba wakikusanya Sh trilioni 1.21 na Oktoba Sh  trilioni 1.29.

Kayombo alisema katika kuhakikisha inaongeza wigo wa kodi, TRA imeweka utaratibu wa kurahisisha upatikanaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Alisema TRA  itakuwa ikishirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)   kumuwezesha mwombaji wa TIN aweze kuipata kwa urahisi.

“TIN inatolewa bure lakini mwombaji atatakiwa kuwasilisha TRA kitambulisho cha taifa na kama atakuwa hana, atatakiwa kwenda NIDA ambako ataweza kupatiwa namba ya kitambulisho cha taifa   imuwezeshe kupatiwa TIN wakati utaratibu wa kupatiwa kitambulisho chake ukiendelea kufanyiwa kazi,” alisema Kayombo.

Alisema sambamba na hilo pia TRA itaendelea kuhamasisha, kutoa elimu ya kodi, kusajili walipakodi wapya katika mikoa, wilaya na vitongoji mbalimbali nchini.

Mamlaka hiyo pia imeanzisha kituo cha ushauri kwa walipakodi kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza ufanisi   na kuongeza ukaribu wa walipakodi na TRA.

Alisema wanatarajia kufungua vituo vya ushari kwa walipakodi katika mikoa mingine lakini pia mamlaka hiyo imeanzisha kampeni rasmi ya usajili wa walipakodi wapya nchini na kuwapa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Katika hatua nyingine, TRA imewakumbusha wamiliki wa majengo kujitokeza kulipa kodi za majengo    kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika siku za mwisho.

Viwango hivyo kwa nyumba za kawaida ni Sh 10,000 wakati   kwa ghorofa ni Sh  50,000 na Sh 20,000 kwa ghorofa za wilayani na vijijini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles