28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yajipanga kukusanya Sh trilioni 23 mwaka 2022/23

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Katika Mwaka wa Fedha wa 2022/2023 Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imelenga kukusanya Sh trilioni 23.65 ambayo ni sehemu ya Serikali ya Sh trilioni 41.4 ikilinganishwa na Sh trilioni 22.99 katika makusanyo ya Mwaka 2021/22.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2022 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema makusanyo hayo asilimia 99.22 ya Malengo yametokana na maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Amesema Rais Samia liwaagiza kukusanya mapato kwa weledi na kukaa na walipakodi kutatua changamoto zao ikiwa kuweka mazingira rafiki ya kulipa kodi.

“Mwaka jana tulizidi kuwekeza kwenye Tehama na uanzishwaji wa Mfumo wa kuwasilisha ritani za VAT kieletroniki ambao umeongeza ufanisi nakuondoa Mapungufu na udanganyifu,” amesema Kayombo.

Amesema katika Mwaka huu wa Fedha wa 2022/23 TRA imelenga kutoa elimu kwa watumishi na wafanyabishara nchini juu ya mabadiliko mbalimbali ya sheria za kodi sambamba na tozo pamoja na ada zinazo simamiwa na taasisi hiyo katika kuratibu taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya serikali.

“Marekebisho haya ya sheria za kodi yamelenga kusaidia kuongeza kasi ya kufufua uchumi na kuimarisha sekta za uzalishaji kwa ajili ya kuboresha maisha,” amesema Kayombo.

Kayombo amesisitiza kuwa katika mwaka huu wa fedha TRA imelenga kufanyia marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa sura 147, sheria ya magari ya kigeni sura 84 sheria ya kodi ya apato sura 332 na sheria ya ongezeko la thamani sura 148.

Ameogeza kuwa sheria zingine ni pamoja na sheria za usimamizi wa kodi sura 438, sheria ya madini sura 123 , sheria usafirishaji bidhaa nje ya nchi sura 196, sheria ya posta na mawasiliano ya kieletroniki sura 306, sheria usimamizi wa forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya 2004 na sheria nyingineza mapato ya siyo ya kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles