Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) ambao kimsingi ndio wanaohusika na usajili wa magari, imesema haiwezi kuzungumzia namba za gari lililotumika kumteka na kumrejesha mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Kauli hiyo ya TRA ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alipotafutwa kwa njia ya simu na gazeti hili lililotaka kufahamu usajili wa gari namba T 314 AXX ambazo zilionekana katika gari lililotumika kumrejesha Mo jana.
Namba hizo ambazo zinaonekana kusajiliwa hapa nchini, ni tofauti na zile alizozitaja juzi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro ambazo ni AGX 404 MC.
Ingawa si Sirro wala mamlaka yeyote iliyotaja nchi iliyo…
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.