26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRA waichanganya TFF, yabeba mabasi

2NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepiga hodi tena katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), safari hii wakiondoka na mabasi yanayomilikiwa na shirikisho hilo kufidia deni la bilioni 1.6.

Mara ya kwanza TRA Kanda ya Ilala iliitikisa TFF kwa kuzuia akaunti zake na kukomba fedha zote kwa madai ya kulipwa fedha wanazoidai ikiwa ni kodi kwa kipindi cha mwaka 2010 – 2015, sehemu kubwa ikiwa ni makato kwenye mishahara (PAYE) ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen, Mart Nooij   na Jacob Michelsen na vilevile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazil uliofanyika mwaka 2010.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, alikiri TRA kuchukua mabasi hayo akieleza kuwa hali hiyo imewachanganya sana na wanachoona kila kitu sasa watakichukia.

“Walikuja watu wa kampuni ya Yono auction Mart kuyakamata mabasi hayo, lakini sidhani hata thamani yake inaweza kufika bilioni 1.6 na kama hali ikiwa hivyo sitashangaa kuona Uwanja wa Karume ukichukuliwa au kupigwa mnada kutokana na deni hilo.

“Kwa TFF hiki ni kilio kikubwa sana,  kama mtu yupo msibani halafu mwingine anakuja kuchukua kirago cha kulalia ni hatari, tunasikitika tumechanganyikiwa,” alisema Malinzi.

Hata hivyo, Malinzi alisema kuwa fedha za makocha ambazo zinadaiwa kodi na TRA, zilikuwa zikilipwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha.

“Hali ya TFF kila mtu anaifahamu ilivyo, juzi tulicheza mchezo dhidi ya Chad ugenini tulitumia zaidi ya milioni 300 na baada ya kurejea nyumbani tulipokea wageni kwa maana ya waamuzi wa kimataifa, tukawapeleka hoteli kula  na kuwalipa hata kama mpira haukuchezwa,” alisema Malinzi.

Pia Malinzi alidai kutodaiwa katika maandalizi yote ya timu ya taifa baada ya kulipa posho zote kwa wachezaji na makocha huku akisisitiza kwamba kwa kipindi kifupi TFF ilitumia zaidi ya dola 300, 000.

Aliongeza kuwa matumizi hayo yakiwa sambamba na kuiandaa timu ya taifa, kuipeleka nchini Chad na kuihudumia ikiwa kambini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles