28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TRA hamumsikii Rais Magufuli ama mna kiburi?

 KAMA kuna jambo naweza kujipongeza kwenye kazi yangu hii ya uandishi basi ni pale siku ninapoandika jambo kuhusu Watanzania wa hali ya chini na nikapigiwa simu na baadhi ya watu kunipongeza kwa kupaza sauti yangu kwa niaba yao.

Moja kati ya kazi hizo nilizowahi kufanya nikajisikia faraja  nimakala niliyowahi kuandika kwa maofisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato (TRA) namaafisa biashara wa manispaa juu ya taratibu zao za tozo na malipo kwa wafanyabiashara.

Makala ile iliwagusa watu wengi sana na hilo nililithibitisha baada ya kupokea simu na ujumbe zakutosha. Ni muda umepita tangu niandike makala hiyo na mambo mengi yanaonekanakubaki vile vile na hiyo ndio changamoto tunayokutana nayo katika kuandika,kwamba kuandika jambo  ni jambo mojalakini kwa mtu kusoma na kufuata ushauri wako ni jambo jingine na hiyo ndiosababu ambayo hufanya waandishi tuonekane ni wapiga domo.

Jumatatu ya Disemba 10, mwaka huu nilikuwa nafuatilia hotuba ya Mheshimiwa Rais alipokuwa amekutana na wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mawaziri pamoja na wakuu wa mikoa mbalimbali lengo likiwa ni kujadili namna ya kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Wakati nafuatilia hotuba yake kuna jambo limenifikirisha sana na kunifanya nijiulize hivi hawa TRA hawamsikii Mheshimiwa Rais ama wana kiburi?

Hii si mara ya kwanza kumsikia Mheshimiwa Rais akiwapa maagizo TRA na kuwaelekeza nini cha kufanya namoja ya maelekezo ni wao kuacha kuwabambikia wafanyabiashara  kodi kubwa inayowafanya kushindwa kulipa nakufunga biashara huku wengine wakisita kabisa kwenda TRA ili wafanyiwe makadirio.Mwezi Machi mwaka huu Mheshimiwa Rais alizungumza hivi “TRA muangalie kodi zenu inawezekana nyingine ni kubwa kuliko miradi ya wananchi, badala ya kuwa motisha inakuwakero, mjipange vizuri, kodi za nyumba mmeenda kutoza mpaka laki sita mpaka milioni wakati tuliwaambie mpige flat rate,”

Ni zaidi ya miezi tisa tangu kauli hiyo itoke kinywani mwa Mheshimiwa Rais lakini bado mambo ni yale yale, awali nilidhani ni sisi tu ambao hatusikilizwi kumbe si hivyo mpaka Rais nayehasikilizwi? Na kwa kuthibitisha hilo hivi juzi Mheshimiwa amerudia tena manenoyale yale “Yapo malalamikokutoka kwa wananchi kuhusu viwango vikubwa vya kodi wanavyotozwa, hususani kwenye sekta ya majengo na hii ndio sababu mapato ya sekta hii yanayokusanywani madogo,” akaendelea  “HaiwezekaniWatanzania tuko milioni 55 halafu idadi ya nyumba zinazolipiwa kodi ziwe milioni moja na laki sita,”  Kauli hii yaRais Magufuli ya Disemba, 10 haina tofauti na ile ya Machi sasa tuwaulize TRAni kwamba hamumsikii Mheshimiwa Rais ama mmekuwa viburi?

Mheshimiwa Rais hakuishia hapo akazungumza na haya

“Kumekuwapo na tatizo la kubambikizia watu kodi kupitia mfumo wa kukadiria kodi. Mtu ana biashara ndogo, anakadiriwa kodi kubwa, mwisho wa siku mtu anafunga biashara yake, sasa hapo TRA mmepata faida au hasara? Wengine hufunga biashara na kwenda kufungua upya,” Hapa kuna neno la kuongeza kweli? Haya makadirio tunayaimba kila siku lakini mambo ni  , naomba niulize tena hivi TRA hamumsikii Mheshimiwa Rais ama mmekuwa viburi? Lakini Mheshimiwa hakuishia hapo akaendelea kwa kusema

“Baadhi ya watumishi wanawalazimishia kodi kubwa wafanyabiashara wadogo na kuwafanya wafunge biashara zao,” Na huu ndio ukweli mchungu.

Moja ya vitu ambavyo vinaniumiza ni kuona tukio la kulipa kodi linavyogeuzwa kama uhalifu, yaani Watanzania kwetu kulipa kodi ni kama kujiingiza kitanzi maana unaweza kwenda TRA lakini utakayokutana nayo huko hutoapa kurudi sasa huu si uzalendo maana uzalendo ni pamoja na kulipa kodi ila kama maafisa hawatufanyi kuona hivyo kwa nini tulipe?

Kiukweli wananchi wamekata tamaa na wengine wanaenda mbalikwa kusema Rais anafahamu nini kinachoendelea haya mengine ni janja janja,maana kama Rais anasema na hayatekelezwi hiyo ni ishara kuwa anafahamu nini kinachoendelea na kwa maana hiyo kwa TRA kutofuata ayasemayo mkuu huko nikumuhujumu mkuu wa nchi hivyo matarajio yetu ni kuwa mtayashughulikia mara mojakwa sababu nina uhakika kuwa mmemsiki na nyie si viburi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles