25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TPA YAJIVUNIA MIZIGO YA RWANDA KUONGEZEKA

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Na KOKU DAVID – DAR ES SALAAM

MIZIGO katika Bandari ya Dar es Salaam imeongozeka katika robo ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 na kufikia tani 228,655 ikilinganishwa na lengo la kuhudumia tani 212,500.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam juzi na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ongezeko hilo ni sawa na tani 7,155 au wastani wa asilimia 3.2 ya lengo.

Taarifa hiyo ilisema hali hiyo inaonyesha kuwa juhudi za TPA kuvutia mizigo kutoka Rwanda zimeanza kuzaa matunda, kutokana na kuongezeka kwa mizigo inayosafirishwa kwenda nchi hiyo jirani ikitokea Bandari ya Dar es Salaam.

“Katika kipindi cha robo ya kwanza (Julai-Septemba, mwaka huu) cha mwaka wa fedha wa 2016/2017, mizigo iliyohudumiwa ilikuwa na tani 228,655, ikilinganishwa na lengo la tani 212,500, ikiwa ni ziada ya tani 7,155 au asilimia 3.2 zaidi ya lengo.

“Mizigo iliyoshughulikiwa katika kipindi kama hicho ilikuwa zaidi ya tani 211,095 za Julai hadi Septemba, mwaka jana, ndani ya mwaka wa fedha wa 2015/2016,” ilisema taarifa hiyo.

Pia ilisema kuwa mizigo iliyofanyiwa kazi kwa soko la ndani katika kipindi hicho cha robo mwaka ni tani 2,482,144 dhidi ya lengo la kuhudumia mizigo yenye tani 1,800,000, huku ufanisi unaonyesha umeongezeka kwa asilimia 37.9.

Aidha, kwa mujibu wa TPA, katika kuhakikisha kasi ya utoaji mizigo bandarini inaongezeka, Tanzania imepunguza vituo vya ukaguzi kutoka 23 hadi vitatu na kwamba hivi sasa utoaji wa huduma bandarini unachukua siku tatu kufikisha mzigo Rusumo kutoka Bandari ya Dar es Salaam, ikilinganishwa na awali ilikuwa ikichukua siku saba.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa katika kuhakikisha Tanzania inaweka mazingira mazuri ya biashara na Rwanda, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, hivi karibuni alitembelea na kukutana na jumuia ya wafanyabiashara wa nchi hiyo na kujadiliana kuhusu changamoto wanazokumbana nazo pindi wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles