Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imesema inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa kiwango cha akiba maalumu (fixed deposit)ili vijana waweze kujiajiri zaidi.
Imesema kiwango hicho kimekuwa ni changamoto kubwa kwa watoa huduma za bima kwa sababu gharama yake ni kubwa.
Akizungumza na Mtanzania Digital leo katika maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF), Meneja wa TIRA, Frank Fred amesema lengo la kutoa kiwango hiko ni kutaka kuona sekta ya bima inakua zaidi na watu kutoa huduma kwa watu wengi na iliyo bora.
Fred amesema ghalama ya kujiunga kuwa wakala wa bima ilikuwa ni sh.milioni 1.8 wameiondoa baada ya kusikiliza ushauri wa Serikali ikiwemo wadau wa sekta hiyo.
“Tunatekeleza agizo la Rais na tinamuunga mkono kwa juhudi anazozifanya katika kuendeleza ajira za vijana,” amesema Fred.
Ameongeza kuwa Al hivi sasa wana makampuni wa wakala zaidi ya 32 ambapo kila kampuni kama itatoa ajira 100 kwa vijana kunakuwa na ajira 302 ambapo itapunguza tatizo la ajira .
Pia katika katika maonyesho hayo ya 46 wamekuja kuwafahamisha wadau wa sekta ya bima kuwa wameanzisha muongozo kwa makampuni ya simu kuweza kuingia ubia kwa wadau wa bima kwa kutumia simu za mkononi .
Aidha, kupitia maonyesho hayo TIRA itatoa mafunzo kwa wadau wao ambao watakaopita katika banda lao kuhusu muongozo wa bima ya takafu ambayo itakayowawezesha watu wa dini zote kitumia muongozo huo.
“Watu wengi wanadhani huu muongozo wa bima ya takafu upo kwa ajili ya waislamu lakini si kweli watu wote wanatakiwa kutumia bima hiyo,” amesema.