26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tigo Pesa yazindua ‘Tigo Pesa Mastercard’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mtandao wa Tigo Pesa kwa kushirikiana na Mastercard na Selcom imezindua rasmi kadi mtandao ili kuwezesha malipo na manunuzi mtandaoni.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema kuwa huduma hiyo ni muendelezo wa kuwarahisishia wateja wao kuendelea kuishi maisha ya kidigitali kwa kufanya manunuzi mtandaoni.

“Huduma hii ni muendelezo wa kuwarahisishia wateja kuendelea kuishi maisha ya kidigitali kwa kufanya manunuzi mtandaoni,” amesema Pesha.

Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji amesema kuwa: “Selcom kwa kushirikiana na Tigo tunawapa wateja wa Tigo uhakika wa malipo popote pale walipo kupitia huduma mpya ya Tigo Pesa Mastercard ili kulipia mambo yote mtandaoni,” amesema Hirji.

Naye Mwakilishi kutoka MasterCad Oyuga Lenin amesema kuwa: “Tunajivunia kushirikiana na Tigo ili kuwapa nafasi wateja wa Tigo kufanya malipo mbalimbali mtandaoni kirahisi na haraka,” amesema Lenin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles