23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tigo Music yawabeba wasanii wa Bongo

bellaNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MUZIKI wa kizazi kipya maarufu kama ‘Bongo Fleva’ ulikuwa haujulikani na haukuonekana kama ni sanaa halisi ya muziki.

Hivi ndivyo ambavyo vizazi vilivyotangulia vilivyoutazama takribani miongo miwili iliyopita japo ni muziki wa kuburudisha watu wa rika zote, wadogo kwa wakubwa.

Muziki wa Bongo Fleva umebadilisha himaya ya muziki Tanzania ambao umepata sifa katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika na Ulaya.

Ni ukweli kuwa sekta ya muziki wa kizazi kipya imekuwa kwa kasi na hata kuwapatia ajira vijana wengi wa Kitanzania wenye vipaji ambao walikuwa hawana kazi nchini kufuatia tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto kwao.

Ingawaje fani ya muziki imekuwa ikionekana kuwa na maendeleo yanayosuasua kwa kipindi cha muongo mmoja hivi, wasanii wa muziki bado wanakumbana na changamoto nyingi.

Wasanii hao wameeleza changamoto hizo kuwa ni mapungufu ya kuwezeshwa kitaifa na kimataifa na kuwepo kwa ujuzi mdogo miongoni mwa wanamuziki.

Kuna baadhi ya makampuni, mashirika na hata watu binafsi ambao wameona umuhimu wa kutatua matatizo kama haya yanayowakabili wasanii na wanamuziki  nchini, badala yake wamegundua mikakati ya kuwawezesha ili kutimiza malengo na ndoto zao kwa ujumla.

Tigo Tanzania ni moja ya makampuni hayo, kwa kuwa ni kampuni ya kidijitali inayobadili maisha ya watumiaji mtandao wake, kampuni hii ilianzisha jukwaa la wanamuziki wa kizazi kipya ijilikanayo kama ‘Tigo Music Platform’  ambayo ina lengo la kuwawezesha wasanii wa muziki nchini na kufanya kazi zao zijulikane ndani na nje ya nchi.

Hadi sasa Tigo imewawezesha wanamuziki wa Kitanzania wapatao 20 kupitia programu yake ya Tigo Music Platform tangu ilipoanzishwa Januari 2015.

Baadhi ya wanamuziki ambao wamefaidika na programu ya Tigo Music wanasema kupitia jukwaa hilo, wasanii wa Tanzania wamejulikana kimataifa.

“Kwa kupitia mtandao huu, wasanii wa muziki wa Kitanzania wamepata fursa ya kujulikana kimataifa, vile vile kupata fedha za ziada kutokana na muziki wao,  hii ndiyo ilikuwa lengo kuu la kuanzisha mtandao huu unaowaunganisha na washabiki.

“Ni matumaini yangu kuwa msaada wa Tigo utaendelea kuwasaidia wanamuziki wa Tanzania katika kukuza fani ya muziki nchini,” anasema mawanamuziki nguli Christian Bella.

Kwa upande wake msanii David Genz maarufu kama ‘Young Dee’, anasema kuwa programu ya muziki wa Tigo Music imemuwezesha kujulikana katika nyanja ya kitaifa na kimataifa.

“Kuanzishwa kwa programu ya ‘Tigo Music Platform’ ni ukombozi kwa wanamuziki wachanga wanauibukia hapa nchini kwa kuwa imetuwezesha kujulikana kimataifa, tunaishuukuru kampuni ya Tigo Tanzania kwa kutusaidia,” anasema.

Tigo Music ilizinduliwa Januari 2015, ambapo Meneja wa Nembo wa Tigo,  William Mpinga, alisema kuwa ina lengo la kukuza kazi za wanamuziki na kuendeleza ukuaji wa soko la wanamuziki wa ndani.

Tigo inasema kuwa, programu ya Tigo Music pia inatoa mafunzo kwa wanamuziki ili kuwajengea uwezo wasanii wa muziki hasa wa kizazi kipya wanaoibukia ili wajue uhalisia wa mali zao kama muziki kuwa ni mali na masoko pia ili waongeze ujuzi wao na kujenga maisha yao kuwa bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles