24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tiger Woods kurudi uwanjani

Tiger Woods
Tiger Woods

EDINBURGH, SCOTLAND

BINGWA namba moja wa zamani kwenye mchezo wa Gofu, Tiger Woods, amedai kuwa anafanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutaka kurudi kwenye mashindano.

Nyota huyo ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na mgongo, amedai kwa sasa anaendelea vizuri na ana mpango wa kutaka kushiriki kwenye michuano mikubwa ya Hero World Challenge.

Bingwa huyo mara 14 katika gofu, juzi alikuwa katika viwanja vya Albany Golf Club vilivyopo mjini Edinburgh nchini Scotland.

Woods amekuwa nje ya uwanja kwa miezi 15, mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo, hata hivyo mchezaji huyo aliamini kuwa hawezi kurudi katika hali yake ya kawaida na kuweza kurudi uwanjani.

Kutokana na hali hiyo kuendelea vizuri, ameweka wazi kuwa atashiriki kwenye michuano hiyo mikubwa ya Hero World Challenge.

“Nimekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, ninaamini mambo mengi yamebadilika kwa kipindi hicho ambacho nimekuwa nje, mwili wangu umebadilika, vifaa, ratiba za mazoezi na mambo mengine mengi, lakini nina hakika nitafanikiwa kurudi katika ubora wangu.

“Naweza kusema mwaka huu umekuwa nafuu kwangu tofauti na mwaka jana ambapo ilikuwa ngumu kutoka kitandani, muda wote nilikuwa nahitaji msaada, nilikuwa na wakati mgumu kwangu na ndio maana nilisema kuwa siwezi kurudi tena uwanjani.

“Mambo mengi yamebadilika kwa sasa, Nike wamejitoa katika kudhamini vifaa vya michezo,” alisema Woods.

Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kuwa hana mpango wa kutangaza kustaafu gofu kwa sasa kwa kuwa bado anaamini kuwa ana nafasi ya kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali.

“Sina ratiba ya kustaafu kwa sasa, ninahitaji kuendelea kupambana kwenye mchezo huu ili niweze kuendelea kuchukua mataji,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles