23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

THRAPA chaomba Serikali kuwasaidia kuunda bodi ya wataalamu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Chama cha Rasilimali Watu na Utawala (THRAPA), Gerald Ruzika ameiomba Serikali kuwasaidia kuunda bodi ya watalaamu ya kusimamia maadili ya taaluma na kushughulikia changamoto zao.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam leo Mei 21, wakati wa kufunga mkutano uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa siku tatu ukiwakutanisha mameneja rasilimali watu na utawala ndani na nje ya nchi, Ruzika amesema lengo la chama hicho ni kukuza taaluma na maadili na ufanisi kazini.

“Tuna changamoto nyingi zinazotukabili ikiwemo uchanga wa chama, tumekuwa na vikao viwili tangu kuanzishwa huu ni mwaka wa tatu na kutokuwa na bodi ya watalaamu, hivyo viongozi tunaomba mtusaidie kutusemea serikalini,”amesema Ruzika.

Amesema changamoto nyingine taaluma yao bado haitambuliki rasmi na kufanya kazi wasio na taaluma ya rasilimali watu na utawala.

Ruzika amesema mkutano huo ulikuwa na ajenda nyingi na nyeti walizokuwa wakijadili na kukubaliana na wanachama.

Nae, Rais wa Chama cha Rasilimali Watu na Utawala wa Afrika Kusini, Profesa Kgothatso Shai amesema rasilimali watu na utawala ni mtu mhimu na anasimamia masilahi ya wafanyakazi.

Nae Rais wa Chama cha Rasilimali Watu na Utawala cha Malawi, Godwin Ng’oma amesema rasilimali watu na utawala ni mtu anayeweza kuunganisha watu katika kazi.

Upande wake mgeni rasmi aliyefunga mkutano huo Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kassinge amesema tasnia hiyo ya rasilimali watu na utawala imepiga hatua nchini.

“Ni kweli hapo nyuma kila mtu alikuwa anafanya kazi ya HR lazima tutambue uwepo wa tasnia hii watake wasitake tutaendelea kusukuma malengo yetu kwa nafasi zetu tulizonazo,”amesema Kassinge.

Amesema kwa umoja huo malengo yao yanaenda kufanikiwa.

Kassinge amesema changamoto zinatambulika katika taasisi wana jukumu la kusimamia masilahi ya watu na maswala yao yote yatarekebishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles