28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TFF yadai nafasi ya Manji kugombewa kama kawaida

Na ZAITUNI KIBWANA

Siku moja baada ya Baraza la wadhamini wa Yanga kusema kuwa Mwenyekiti wao, Yusuph Manji amerejea, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ally Mchungahela ameibuka na kudai kwamba uchaguzi wa viongozi wa timu hiyo upo pale pale ikiwemo nafasi ya Manji.

Akizungumza na MtanzaniaDigital, wakili huyo amesema nafasi ya Manji ni miongoni mwa nafasi zinazowaniwa kwenye uchaguzi huo.

“Sisi uchaguzi unaendelea kama kawaida na hata nafasi ya Manji pia watu wanachukua fomu kama tulivyoelekezwa na serikali,” amesema.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika January 13 mwaka huu baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu Mei 2017.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles