26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Teknolojia katika viwanda itainua uchumi

rweyemamu 3NA MAREGESI PAUL, OUT

KUKUA kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kumeleta mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku.

Mafanikio haya yanathibitika kutokana na kuongezeka kwa huduma za mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi katika jamii.

Mabadiliko ya teknojia yanajitokeza kila siku hadi siku duniani na kubadili mitindo ya maisha na utendaji wa kazi katika sekta na taaluma mbalimbali.

Wapo baadhi ya watu makini ambao wakati wote wamekuwa wakifuatilia mabadiliko hayo ili kuhakikisha hayawaachi nyuma.

Miongoni mwa wafuatiliaji wa mabadiliko ya kiteknolojia na anayeamini kuwa bila kutumia teknolojia za kisasa hususani katika uzalishaji wa viwanda si rahisi kufanya uzalishaji wenye tija na ufanisi ni Mhandisi Salvatory Rweyemamu.

Rweyemamu ambaye ni Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Arusha na Kiwanda cha kusindika Shayiri cha TBL kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro, amasema pamoja na majukumu mengi ya kazi aliyonayo huwa anahakikisha anasoma mambo mbalimbali kuhusiana na teknolojia mpya zinazoibuka kila kukicha duniani kote ili kuhakikisha anakwenda sambamba na mabadiliko hayo.

“Naipenda taaluma yangu ya uhandisi wa umeme kwa kiasi kikubwa, muda wangu mwingi huwa nautumia kusoma mambo mengi yanayohusiana na fani hii kwa kuwa teknolojia duniani inakuwa kwa kasi kubwa.

“Ukitaka kuwa mtaalamu na kufanya kazi kwa ufanisi na kwenye kampuni kubwa kama nilipoajiriwa unahitaji kuhakikisha muda wote unakwenda na wakati hususani kujua mabadiliko ya kiteknolojia yanayotokea kila kukicha,” anasema.

Anasema mara nyingi huwa anawaza ni jinsi gani  wasomi wa fani ya sayansi nchini wanaweza kutumia taaluma zao kuleta mabadiliko kwenye jamii na kufanya ubunifu wa kiteknolojia badala ya kutegemea ubunifu wa wataalamu wa nje ambao kila  kukicha wanaleta mambo mapya ambayo watu wanayatumia na kuyafurahia hata mengine yakiwa si mazuri.

Rweyemamu anasema alipata elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) ambako alisomea shahada ya kwanza ya uhandisi wa umeme na alikuwa miongoni mwa wahitimu waliofanya vizuri mwaka 1988.

Baada ya kumaliza masomo aliajiriwa na Kampuni ya TBL katika kiwanda cha Ilala akiwa kama mhandisi wa umeme.

“Baada ya kufanya kazi kwa kipindi kifupi nilibahatika kupata nafasi ya masomo ya shahada ya uzamili nchini Ujerumani nikiwa nimejikita zaidi katika uhandisi wa umeme wa viwandani na mitambo inayotumia teknolojia za kisasa,” anasema.

Anasema baada ya kurejea nchini aliendelea kufanya kazi za uhandisi katika kiwanda cha TBL na kupandishwa cheo kutokana na ufanisi wake mpaka kufikia nafasi aliyonayo akiwa Meneja anayesimamia viwanda viwili.

Meneja huyo anasema tayari amehudhuria kozi mbalimbali za ndani ya kampuni  ambazo zimezidi kumpatia maarifa katika fani yake na kumfanya awe miongoni mwa wahandisi nguli wanaoaminika nchini katika fani ya uhandisi wa umeme na uendeshaji wa mitambo ya kisasa.

“TBL kuna mafunzo ya aina nyingi na kuna mitambo ya kisasa, mara nyingi tumekuwa tukipata mafunzo ya aina mbalimbali  ikiwemo ya mifumo ya uendeshaji viwanda kwa ufanisi.

“Kwa mfano ‘SABMiller Manufacturing Way’ ambayo tunaitumia na imeonyesha mafanikio makubwa na kufanya viwanda vyetu kuwa na uzalishaji wenye tija,” anasema.

Pia anasema anaweza kufanya kazi zake vizuri kutokana na ushirikiano mzuri anaopata kutoka kwa wafanyakazi wenzake.

“TBL ni tanuru la kupika wataalamu na imeajiri watu wenye uwezo mkubwa katika fani zao, hivyo nafanya kazi na wataalamu ambao wana upeo mkubwa na wanaoelewa nini wanachokifanya bila kuhitaji usimamizi mkubwa,” anasema.

Mhandisi Rweyemamu anasema anajivunia kufanya kazi na kampuni kubwa kama TBL ambayo imemuwezesha kujifunza mambo mengi ikiwemo kupata mafanikio mbalimbali katika maisha yake na kuweza kuihudumia familia yake vizuri.

Malengo yake ya baadaye baada ya kustaafu kazi ni kujiajiri kwa kufanya kazi za ushauri wa kitaalamu wa fani ya uhandisi umeme ambayo anaamini kuwa inazidi kukua na kuhitaji wataalamu tofauti na ilivyokuwa  miaka ya nyuma.

Rweyemamu anatoa wito kwa vijana wa kitanzania kutokimbia masomo ya hesabu ya sayansi wanapokuwa mashuleni bali wajitahidi kuyazingatia kwa kuwa  katika dunia hii ya sayansi na teknolojia bila wataalamu itakuwa vigumu kwa taifa kupiga hatua ya maendeleo.

“Vijana wengi wa siku hizi wanakuwa si wavumilivu na wanapanga malengo makubwa ambayo inakuwa vigumu kuyafikia kwa muda mafupi, matokeo yake wanajikuta wamejiingiza kwenye vitendo vya wizi na kuwaibia waajiri wao hali inayosababisha wasiaminike.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles