25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

TCU YATAKIWA KUANDAA MAWAKALA VYUO VYA NJE

Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM

TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imeshauriwa kuandaa orodha ya kampuni za mawakala wa vyuo vikuu vya nje ambazo zinatambulika ili kuondoa udanganyifu wanaofanyiwa wazazi.

Akizungumza katika mkutano wake na wadau wa elimu, Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, alisema kumeibuka kampuni nyingi za kitapeli zinazodai kuwapeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi kinyume na utaratibu.

Alisema kuibuka kwa matapeli hao kunawasababishia kutoaminiwa na wazazi hivyo ameiomba TCU kuzitambua kampuni zote.

“Niiombe TCU kuweka orodha ya kampuni za mawakala wanazozitambua katika mtandao wao kuwasaidia wazazi kuepukana na utapeli,” alisema Mollel.

Alisema GEL wameamua kukutana na wadau wakiwamo TCU, wazazi na wanafunzi wanaosoma nje ya nchi ili kujadili kwa pamoja maswali ambayo wazazi wamekuwa wakijiuliza.

“Tutawaondoa hofu ya maswali yao wanayoyauliza kila siku yakiwamo lini watoto wataondoka nchini, usalama wao wakiwa huko, watafikia wapi na upatikanaji wa vibali kutoka TCU,” alisema Mollel.

Naye Ofisa Habari mwandamizi kutoka TCU, Edward Mkaku, aliwaonya wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi kuepuka kujihusisha na makundi ya uhalifu ambayo yatawasababishia kushindwa kuendelea na masomo yao.

Alisema waige mila na desturi njema zilizopo katika nchi hizo, lakini wasiige maovu.

“Huko mnakokwenda mtakutana na makundi mbalimbali yakiwamo ya wauza dawa za kulevya, viungo vya watu na mengineyo jihadharini kujiingiza huko,” alisema Mkaku.

Aliitaka GEL kufuatilia mienendo ya watoto wakiwa masomoni ikiwa ni pamoja na kupata taarifa kutoka katika vyuo wanavyosoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles