24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA yatoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mara kuelekea Uchaguzi

Na Malima Lubasha, Musoma

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari mkoani Mara juu ya kanuni na Sheria za utoaji Habari hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

Akizungumza juzi mjini Msoma, Meneja Mawasiliano Kanda ya Ziwa (TCRA), Mhandisi Imelda Salumu amesema mada mbalimbali zilizowasilishwa na wawezeshaji katika warsha iliyofanyika mjini Musoma inalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwa kuwaongezea uelewa ili wasikiuke sheria na maadili ya uandishi habari kuelekea kwenye uchaguzi huo unaotarajwia kufanyika baadae mwaka huu.

“Hii ni fursa muhimu  ya kuwakumbusha wanahabari kuzifahamu vizuri kanuni,sheria na maadili wakati wanatekeleza majukumu yao kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka kesho waweze kutangaza na kuwasilishwa kwa kuwaandaa wananchi kuwa tayari kupokea taarifa hizo zilizo sahihi,” amesema Mhandisi Salumu.

TCRA pia imetumia warsha hiyo kuwakulbuha waandishi wa habari kujisajili ili waweze kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria.

“Wito wangu kwa wanahabarikuwa  katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuna watu wengi wanajitokeza kuingia kwenye hii tasnia bila kufuata utaratibu na sheria zilizowekwa niwaombe wale wanaopeleka  maudhui mitandaoni ambayo ni habari unapaswa kuwa leseni kutoka TCRA,” amesema Mhandisi Salumu.

Naye Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza Press Club amesema lengo la semina ni kuwapitisha waandishi wa habari mkoani hapa kuzijua kanuni za uchaguzi na maadili na mambo gani wanapaswa kuyafanya.             

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles