27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tchisekedi kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa

KINSHASA, DRC

RAIS mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi, amesema atawaachia huru wafungwa wote wa kisiasa.

Wafungwa hao ni pamoja na wale waliofungwa wakati wa maandamano yaliyofanyika kabla ya uchaguzi wa mkuu Desemba mwaka jana.

Tshisekedi alikuwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi ulioigawa nchi kutokana na shutuma za wizi wa kura ili kuwazuia wakosoaji wa Rais Joseph Kabila kuingia madarakani.

Katika hotuba yake aliyoitoa jijini hapa juzi, Tshisekedi, alisema ”Nitamuomba waziri wa sheria kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa waliowekwa gerezani kutokana na tofauti ya maoni.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo, miongoni mwa wafungwa hao huenda ni wafuasi wake’.

Katika uchaguzi wenye utata wa Desemba mwaka jana, Tshisekedi alidaiwa kushika nafasi ya pili nyuma ya mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu lakini akapewa ushindi baada ya kufanya makubaliano na Kabila.

Hata hivyo, Mahakama ya Katiba ilimuidhinisha rasmi Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo baada ya kukataa ombi la rufaa liliwasilishwa na Fayulu.

Wito wa Tshisekediwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa unaonekana kama pigo kwa mtangulizi wake.

Ikiwa wataachiwa huru kweli au la , itakuwa ni kipimo cha mamlaka aliyonayo Tshisekedi, ambaye kuna wasiwasi ya kuendeshwa kama ripoti na mtangulizi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles