30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Trump adai kuna njama kumuondoa madarakani

MARYLAND, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump amewashambulia vikali wapinzani wake akisema wamepanga kumuondoa madarakani.

Akizungumza katika mkutano wa Chama chake cha Conservative jimboni hapa jana, Trump alisema ripoti malumu ya uchunguzi ya Robert Mueller na wakosoaji wengine ni njama za kumhujumu.

Katika hotuba inayotajwa kuwa ndefu zaidi katika utawala wake, Trump alisisitiza hana uhusiano wowote na madai ya muingilio wa Urusi katika kampeni yake.

“Tunasubiri ripoti ya watu ambao hawakuchaguliwa”, aliuambia umati wa wanachama wa Conservative waliokuwa wakimshangilia.

Mueller anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa mwendesha mashtaka mkuu muda mfupi ujao.

“Kwa bahati mbaya mnaweka watu wasiofaa katika nafasi kadhaa za uongozi, na watu wamekuwa wakilalamikia uwepo wao kwa muda mrefu na sasa wanapanga njama ya kukuondoa madarakani. Ni sawa hii?” alihoji.

“Hivi ndivyo nilivyoteuliwa, kuzungumza bila mwongozo maalumu . na tusipofanya hivyo nchi yetu inaelekea pabaya wenzangu,” alianza kusema.

Mara kadhaa Rais Trump alisema Robert Mueller hakuwahi kuchaguliwa, na kwamba ni Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu Rod Rosenstein, aliyemweka Mueller katika nafasi yake.

Kuna madai Rosenstein huenda akajiuzulu kutokana na mashambulizi ya rais ya mara kwa mara dhidi yake.

Rais Trump alidai Mueller alikuwa rafiki yake mkubwa huku akimkejeli Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI), James Comey aliyemfuta kazi Novemba mwaka jana.

Alisema Sessions alikuwa alikuwa mdhaifu na hakuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake ilivyostahili.

Rais pia alitaja pendekezo jipya la chama cha Democratic kuhusu masuala ya kuimarisha tabia nchi la kulinda kuwa wazo la ajabu, akisema upepo utakapoacha kuvuma huo utakuwa mwisho wa umeme.

Baada ya kugusia masuala kadhaa kuhusu wahamiaji, alisema lazima tupende nchi yetu. Bungeni tuna watu, ambao hawaipendi nchi yetu”

“Najua mnafahamu hilo na tunaweza kuwataja wote kwa majina yao tukiamua kufanya hivyo,” alisema.

Pia alitetea mkutano wake na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un, aliosema kuwa umepiga hatua kubwa.

Hotuba hiyo inakuja wiki moja baada ya wakili wake wa zamani Michael Cohen, kudai kiongozi huyo alimtaka adanganye kuhusu kuhusu ujenzi wa jengo lake mjini Moscow wakati wa kampeni ya uchaguzi wake 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles