30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

TCAA yatathimini utayari wa kukabili ajali za ndege

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kufuatia taharuki ya kuanguka kwa ndege maeneo ya Kisarawe mkoani Pwani Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ) imewatoa hofu wananchi juu ya tukio hilo kwamba lilikuwa ni zoezi la kutathimi utayari pindi ajali zinapotokea katika usafiri wa anga nchini.

Akitolea ufafanuzi Julai 27, jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa TCAA, Flora Alphonce amesema tukio hilo lilikuwa ni zoezi ambalo lengo lake ni kupima uwezo na utayari wetu kama nchi wa kukabiliana na matukio ya utafutaji na uokoaji pindi ndege zinazopata ajali kwenye nchi kavu au majini na pia vyombo vya majini.

“Kutokana na utafutaji na uokoaji wa ndege ya abiria iliyoanguka katika kijiji cha Msufini Kidete, Kata ya Mbezi, tarafa ya Shungubweni, Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani ikiwa inatoka katika uwanja wa Kilwa Masoko na kuelekea uwanja Tanga Ndege hiyo aina ya Embraer 120 (E120) ilikuwa imebeba abiria 25 TCAA tuna watoa hofu wananchi kuhusiana na tukio hilo lilikuwa ni zoezi la kutathimi utayari pindi ajali zinatokea,” amesema Frola.

Ameeleza kuwa zoezi hilo lilihushisha vyombo mbalimbali vya uokoaji ni pamoja na Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Zimamoto, Shirika la Msalaba Mwekundu (RED CROSS), Hifadhi za Taifa (TANAPA), TASAC, Jeshi la Polisi, Wavuvi na wadau wengine ili kujiweka tayari pindi ajili halisi zanapotokea kwenye anga la Tanzania.

Amesema zoezi hilo limeandaliwa na TCAA ambalo inajukumu la kuratibu na kusimamia huduma ya utafutaji na uokoaji wa ndege zinazopata ajali kwenye anga la Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi za udhibiti wa usafiri wa majini ambazo Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa Tanzania bara na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini (ZMA) kwa wa upande wa Zanzibar.

“Tanzania imeridhia Mkataba wa Kimataifa wa Utafutaji na Uokoaji Majini wa mwaka 1979 (International Convention on Maritime Search and Rescue, (SAR Convetion,1979) unazungumzia kuhusu masuala ya utafutaji na uokoaji katika usafiri wa majini,” amesema Flora.

Amesema mikataba hiyo yote inayosimamiwa na ICAO na IMO inazitaka nchi wanachama kutoa huduma za utafutaji na uokoaji katika usafiri wa anga na majini wakati ajali na matukio ya dharura ya vyombo vya usafiri wa anga na majini ndani ya eneo la nchi mwanachama.

Kwa upande wa Tanzania, eneo la nchi la utafutaji na uokoaji ni mipaka ya kimataifa ni eneo la Bahari ya Hindi kuanzia pwani ya Tanzania kuelekea Mashariki hadi Longitudi nyuzi 44 (440E) pamoja na maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Amesisitiza kuwa katika utekelezaji wa maelekezo yaliyo katika Mwongozo huo, Tanzania imeimarisha na kuboresha vituo vya kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji katika usafiri wa anga na majini ambavyo Vituo hivyo vinavyojulikana kama Aeronautical Rescue Coordination Centre (ARCC) ambacho kipo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na Maritime Rescue Coordination Centre (MRCC) ambacho kipo eneo la Magogoni, Dar es Salaam. Kituo cha ARCC kinasimamiwa na TCAA na kituo cha MRCC kinasimamiwa na TASAC.

Amesema mwongozo huo wa ICAO na IMO unazitaka nchi wanachama kufanya majaribio au mazoezi ili kupima uwezo na utayari wa taasisi zote zinazohusika katika kutoa huduma hii muhimu ya utafutaji na uokoaji hivyo kufanya mazoezi haya ni kutekeleza matakwa ya sheria na mikataba ya kimataifa ili kuboresha mifumo, taratibu na vifaa vya utafutaji na uokoaji.

Naye Meneja Uhusiano na Mawasiliano TCAA, Yessaya Mwakifulefule amesem zoezi hilo limehusisha waangalizi wa ndani na nje ya nchi ili kutathmini maeneo yanahitaji kuboreshwa ili huduma hii itolewe kwa ufanisi mkubwa.

“Waangalizi hao ni kutoka Shirika la kimataifa la usafiri wa anga duniani (ICAO), Mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi, Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) na Mashirika ya vyombo vya majini. Waangalizi hawa watatoa ripoti ambazo zitafanyiwa kazi ya kamati ya kitaifa ya utafutaji na uokoaji wa ajali za ndege na vyombo vya majini,” amesema Mwakifulefule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles