24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

TBL yaandaa mkutano mkuu wa 51 na kujadili maendeleo na changamoto

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imefanya mkutano wake mkuu wa 51 wa mwaka, ulioshirikisha wadau mbalimbali kujadili maendeleo ya TBL na changamoto zinazokabili kampuni hiyo kwa mwaka wa fedha uliopita.

Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Leonard Mususa, alizungumza na wanahisa wakati wa mkutano huo, ambao uliangazia utendaji wa kifedha wa TBL PLC, mikakati na nafasi yake katika soko.

Mususa alisema kuwa ajenda muhimu katika mkutano huo ilikuwa ni udhinishwaji wa gawio la shilingi 537 kwa kila hisa, jumla ya Sh 158,445 milioni kwa mwaka uliomalizika Desemba 31, 2023. Ongezeko hili la asilimia 85 ikilinganishwa na mwaka uliopita linaonyesha dhamira ya TBL katika kurudisha faida thabiti kwa wanahisa wake.

“Tunajivunia kutangaza kuwa licha ya hali ngumu ya mwaka 2023, ikijumuisha mvutano wa kisiasa kijografia duniani na ongezeko la ushuru wa ndani, TBL PLC inaonyesha ukuaji thabiti na kutoa thamani kubwa kwa wanahisa wetu.

Utekelezaji wetu madhubuti wa mipango ya kimkakati na imani ya soko katika orodha ya chapa mbalimbali ilisababisha ongezeko kubwa la mapato kutuwezesha kuidhinisha na kusambaza gawio la Sh 537 kwa kila hisa, ongezeko kubwa zaidi la asilimia 85 ikilinganishwa na mwaka uliopita,” alisema Mususa.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo inaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibiashara ulio thibitishwa na kuongeza mauzo na masoko nyuma ya orodha ya chapa za bia na zaidi ya bia ili kutoa ukuaji thabiti na kuunda thamani ya muda mrefu. TBL inanunua zaidi ya asilimia 74 ya malighafi zake kutoka ndani ya nchi.

Mususa alisema mwaka 2023 TBL ililipa kodi ya serikali shilingi bilioni 586, ikilinganishwa na Sh bilioni 528 kwa mwaka uliopita, hivyo kampuni hiyo ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa wa Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles