26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

TASAC yaonya vyombo vya mizigo kubeba abiria

Na Yohana Paul, Geita

SHIRIKA la Wakala wa Huduma za Meli Tanzania (TASAC) limewataka watanzania kuacha tabia ya kusafiri kwa kutumia vyombo vya majini vilivyopewa leseni ya kusafirisha mizigo kwani usalama wao upo hatarini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tasac, Mohamed Salum ametoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi kwenye Maonyesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Amesema ipo kasumba ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya majini kwenda kinyume na leseni zao jambo ambalo hupelekea ajali za majini ambazo zingeweza kuepukika kwa kufuata utaratibu.

“Siyo unakuta mtumbwi wa uvuvi unapanda, au unakuta meli imebeba mizigo nawe unapanda, vyombo vya mizigo ni vya mizigo, na vina leseni ya mizigo,” amesema.

Salum pia alikemea tabia ya baadhi ya watu kutumia mawakal amaboa siyo rasmi kuingiza mizigo nchini na kueleza kuwa Taasac inashirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kukomesha tabia hiyo.

“Tasac tuna ushirikiano mkubwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, kupitia kitengo chao cha forodha huwa tunapata taarifa kuna watu wanatumia mawakala ambao siyo Tasac kutoa huduma.

“TRA imekuwa ikiwakatalia na kuwapa maelekezo uingizaji wao lazima upitie Tasac kwa sababu za kiusalama ili serikali iweze kupata taarifa ya vitu vinavyoingia na kutoka,” amesema.

Salum amewataka wachimbaji wa madini wadogo, wa kati na wakubwa kuzingatia miongozo ya uingizaji wa vilipuzi na usafirirshaji wa makinikia hususani wa kupitia Tasac ili kungamua uhalali wa biashara yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles